Saturday, August 23, 2014

WAPENZI NA WATANZANIA WAPENDA MAENDELEO UK TUMESIKITISHWA NA HABARI ZA UPORAJI WA KURA DMV - USA

Watanzania wengi wapenda maendeleo nchini UK tumesikitishwa kutokana na taarifa mbali mbali za kuchakachuliwa kwa kura kufuatia uchaguzi wa Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV uliofanyika tarehe 9/08/2014.

Taarifa za unyang’anyi wa kura katika uchaguzi huo umetokana na malamiko yaliyotolewa na waliokuwa Wagombea katika nafasi mbalimbali pamoja na Jumuiya na Taasisi nyingine. Malalamiko hayo yanahoji utaratibu mzima uliotumika kuanzia kwenye kampeni hadi uhesabu wa kura na hata matokeo rasmi yalivyotangazwa.

Salma Moshi aliyekuwa mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti alitoa tamko rasmi kupinga matokeo hayo kutokana na nafasi za kiupendeleo walizopewa baadhi ya Wagombea katika kujinadi. Nafasi hizo za kiupendeleo zilitumika wakati wa mikutano ya Jumuiya ambayo haikutakiwa kutumika kwa ajili ya kampeni kwa kuwa ingewapa nafasi zaidi Viongozi walioko madarakani lakini hicho ndicho kilichotokea. Barua rasmi ya malalamiko ya Salma yanapatikana hapa Malalamiko ya Salma Moshi

Kwa upande mwinigine aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti, ndugu Liberatus Mwango’ombe na timu yake nzima, imetoa malalamiko yanayoonesha ukiukwaji mkubwa wa zoezi zima la kuhesabiwa kwa kura pamoja na utaratibu uliotumika kutangaza matokeo. Barua rasmi iliyoainisha malalamiko hayo inapatikana hapa:Malalamiko ya Liberatus Mwangombe

Tarehe 14/08/2014 wachungaji wanaoongoza jamii ya waTanzania Washington DC kiroho walitoa tamko rasmi wakieleza kasoro nyingi zilizotokea kwenye uchaguzi huo na kuita matoke yake batili. Tamko rasmi la wachungaji hao linapatikana hapa:Malalamiko ya wachungaji

Kutokana na hali hii, sisi waTanzania wapenda maendeleo nchini UK, tumeshtushwa na taarifa hizi za kirushwa rushwa zilizotokea kwenye nchi inayojali na kuthamini demokrasia. Matagemeo ya waTanzania wengi waliobaki nyumbani Tanzania ni ya kiwango cha juu kwani huwaangalia WaTanzania wa Diaspora kwa mtazamo tofauti wakitegemea uadilifu zaidi na nidhamu nzuri kutokana na uelewa wao wa mambo mengi. Taarifa hii ni tofauti kabisa na mategemeo hayo. Ni aibu siyo tu kwa wana DMV bali kwa Wana-Diaspora wote.

Taarifa hizi ni za kusikitisha na tunaiomba Kamati ya uchaguzi pamoja na Mh. Balozi wa Tanzania nchini USA kutafuta na kuleta suluhu itakayorudisha imani kwa WaTanzania. Hii ni kwa nia ya kurudisha harmony na ushiriki wa kila mtu katika  juhudi zilizopo za kimaendeleo. Ili Jumuiya iweze kufanyaka kazi zake kwa ufanisi na kwa ushikiano wa kila mmoja, ni muhimu sana kwa wale wote wanaohusika kulitazama upya swala hili na kwa umakini zaidi.

Tunaipenda Tanzania na Tunapenda Maendeleo ya WaTanzania

Mungu ibariki Tanzania

No comments: