MCHANGANUO HUU UNAENDELEA KUTHIBITISHA KUWA UCHAGUZI WA AUGUST 9, 2014 NI BATILI
"TOA KURA 15 MARUANI; LIBE ATOSHA"
Tumesoma mchanganuo wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Mzee
Safari na ametoa mahesabu ambayo yanazidi kuongeza sintofahamu. Huu ni mchanganuo wa kutengenezwa ili
kuwapumbaza wana DMV; “Team Libe for DMV President 2014” itathibitish ubatilii huu pasi na shaka. Tunanukuu mchanganuo huo wa Tume hapa
chini. Kama ifuatavyo;
Mchanganuo wa Tume ya
Uchaguzi kutoka kwenye report ya mwisho.
Yafuatayo ni matokeo ya ukaguzi wa mfumo wa kura
uliobainisha hitilafu:
a)Idadi ya wapiga kura walioko kwenye orodha ya wanachama hai: 586. Wanachama 150 waliamua kutopiga
kura.
b) Wanachama waliopiga kura
kituoni: 436
c) Kura za ghaibu
( in absence): 14 Mgawo wake ni: Libe 9 na Iddi 5
d) Kura zilizo toka
kwenye masanduku na kuhesabiwa na mawakala: 445: Katika hizo mawakala wa Libe waliripoti kura 214, na wa
Iddi waliripoti kura 231: Kwa hivyo kuna kura za ziada kwenye
masanduku kuliko idadi ya wapiga kura. Ziada hiyo ni kura 9.
Kutokana na
mchanganuo huu wa kupikwa, naomba msomaji shirikiana na “Team Libe for DMV
Community 2014” ili tuthibitishe udanganyifu wa Tume ya Uchaguzi na Board of Trustee
chini ya Hamza Mwamoyo.
Mzee Safari
anasema; Wanachama hai ni 586, wanachama
ambao hawakupiga kura ni 150; na
waliopiga kura kituoni ni 436. Mzee Safari anaongeza kuwa; waliopiga kura za
ghaibu (absentee ballot) ni 14.
Sasa basi,
shirikiana nasi kufanya mahesabu ya darasa la kwanza kwa kujumlisha waliopiga
kura kituon 436, ambao hawakupiga kura 150 na waliopiga kura za ghaibu (absent) 14; (436+150+14= 600). Rejea hapo juu orodha ya wanachama hai ni 586, lakni jumla
inaonyesha 600: KWA NINI NUMBER
STILL DON'T ADD UP!
Ukichukua kura za ziada 9 (445-436=9) ongeza na wanachama ambao sio hai
14 unapata kura maruhani 23 (9+14). Hii inamaanisha uchaguzi huu ulikuwa na kura BATALI 23.
Napenda kuitaarifu Board of Trustee na Tume ya Uchaguzi kuwa;
wana DMV 223 walio mchagua Liberatus (50% ya walio piga kura) bado wanaomba maelezo juu ya kura 15 batili;
na sasa tunaomba maelezo ya kura 23 BATILI.
Pia, kulingana na mchanganuo huo hapo juu; inaonyesha kuna watu 14 ambao
sio wanachama hai walishiriki kupiga kura.
UCHAGUZI HUU NI BATILI KAMA
ALIVYO SEMA MZEE SAFARI SIKU YA JUMAMOSI AUGUST 9, 2014; TUNAOMBA WANA DMV MSHIRIKIANE NASI KATIKA KUDAI HAKI KWA KUWEKA SAHIHI KWENYE PETITION HII PINGA UCHAGUZI WA AUGUST 9, 2014 NI BATILI
TEAM LIBE FOR DMV COMMUNITY PRESIDENT 2014
No comments:
Post a Comment