Kawaida sio mtu wa
politics ila kwa sababu kadhaa imebidi niingie kuongea yangu mawili matatu
yalionifanya nimpe kura yangu ndugu Libe
kwenye huu uchaguzi wa urais DMV. Na imani kuwa Iddi ni mtu mzuri lakini na hakika
kuwa uongozi huu wa kuongoza hapa DMV hauwezi. Watanzania tunahitaji maendeleo
ktk hii community yetu lakin bado maendeleo hayaonekani. Watanzania tunahitaji
maendeleo kama michongo ya kupata uhalali wa kuishi, kupata kazi, huduma za
afya na mahala pa kuishi kwa urahisi ili hayo mambo mengine ya kufanya vitu nyumbani
Tanzania yawe mepesi.
Ndugu Libe bila kunifahamu aliweza kuni
contact, sio aniombe kura bali ni kuongea nami kuhusu kuindeleza Community
yetu. Akaniomba kuchangia mada katika masuala ya maendeleo ktk community yetu. Alizungumzia
masuala hayo nilioyataja hapo juu. Na alinivutia na sera zake za kutaka
kuwasaidia watanzania waweze kuwa na maendeleo kimaisha. Maelezo na unyenyekevu
wake ulinipa moyo.
Sasa maswali niliokuwa najiuliza kuhusu Uongozi wa Iddi ni
haya:
1. Iddi ananifahamu
na number yangu anayo na kama alipoteza basi angeweza kuipata kwa watu kadhaa
sasa mbona hajadiriki kunitafuta kwa simu japo kuwa nilishaonana nae mara
kadhaa hivi karibuni lakin nilimuona
akinikwepa sasa hii kama si dharau ni kitu gani? Japo kuna wachache wanaodai
kuwa Iddi ni mtu wa kujichanganya kwenye misiba na mashughuli sasa basi kama ni
hivyo wengi wetu walitakiwa kuwa viongozi maana wengi wetu wanakwenda kwenye
kila shughuli. Kiongozi anatakiwa awe na hadhi ya kuongoza, na si sifa ya
uongozi hio ya kuhudhuria tu mashughuli bila kufanya kazi ipasavyo.
2. Miaka miwili
katika uongozi wa Iddi, Community yetu haina hata office, jamani hii si aibu. Je
Iddi aliwahi kutumia jitihada za kutafuta sponsors? Ili kufanikisha hili suala?
Kwa mtaji huu watanzania wata kuwaje na maendeleo. Mfano unaanzisha chama na
tawi halafu hakuna Office, jamani huu kama si utani ni nini? Au unafuga mbuzi
halafu huna zizi. Vile vile mapato na hasara ya jumuiya yalitakiwa yawe wazi
kwa kila mtanzania DMV kushuhudia, ikiwa wewe ni Rais wa watanzania DMV kama
unavyo claim. Sasa wewe na uongozi wako mbona mnaficha matumizi ya Jumuiya? Na
kama wanachama ndo wenye access ambao idadi yao ilikuwa less than ten, Basi hutakuwa
na haki ya kuwa Rais wa wetu DMV.
3. Wengi wetu
wanalalamika kuwa upande wa Libe
kuna wanaotukana wenzao: Mbona mimi kwa macho yangu nimeshuhudia upande wa Iddi
unaporomosha matusi makubwa ya kupasua Jabali na ushahidi upo. Lakini Iddi
anakuwa kimya. Watu wangapi hapa DC
wanatukanana na kugombana kila mara, Je wewe kama kiongozi uliwahi kutoa tamko
lolote kukemea hio tabia au hata kuwaita wahusika na kuzungumza nao. Well
lakini utawaita wapi wakati hakuna Office. Utawaita watu park mpaka lini? Na
kuwaharibu afya zao kwa kuwalisha minyama na mipombe.
4. Nashangazwa na
Iddi kunga’ang’ania madaraka, sasa kama ni kujitolea tu bila mshahara kwa nini
huwapi chance na wenzio? Kwani wenzio hawapendi ku volunteer? Na kama unavyodai
kuwa hujamaliza masuala Fulani fulani; sasa nakuuliza kwani wewe ni Raisi wa
Nchi? Basi isingependekezwa miaka miwili miwili ya uongozi katika katiba
wangeweka minne au mitano kabisa. Na kuhusu hilo darasa la Kiswahili
unalolishadadia, sawa sikatai kuwa lina umuhimu ila nakushangaa kwa nini
hushadadii na madarasa ya kiingereza ambayo yapo bure hapa DMV. Kuna watanzania
wapo hapa miaka zaidi ya kumi lakini kiingereza chao kibovu wanashindwa hata na
mtu alieko Kibaigwa. Ungeweza kuwasaidia kwa kuwa registered na kuwapatia elimu hiyo ya
bure ambayo itawasaidia katika kuendeleza shughuli zao za kila siku.
Namaliza kwa kuwaomba watanzania wenzangu
wanaonifahamu na wasionifamu na kwa wale nilio ishi nao kwa wema tafadhalini mchagueni
Libe muone mabadiliko, na Imani kuwa
ataipendezesha hii Community yetu ya DMV. Na mimi naahidi nitashirikiana nae
kwa hali na mali katika kuleta maendeleo. Watanzania mna ongoza kwa ukarimu na
kupenda amani basi na tuamke pamoja tufanye kitu cha maana. Kama
hujajiandikisha basi leo hii jiandikishe for just $25, Ili uweze kuwa active. Na
kama una swali lolote mpigieni Libe
na uongozi wake wapo kwa ajili ya kila mtu 24/7. Nawaomba tena watu wangu, ndugu
zangu, rafiki zangu na watanzania wenzangu mkienda kupiga kura mpigie Libe. Hio ni haki yako. Shukrani zangu
za dhati kwa Vijimambo Blog na kwa Watanzania wenzangu wote.
Ni mimi Buhite Jabry
No comments:
Post a Comment