Tunapenda kutoa taarifa kwa Umma wa DMV kuwa, Team Libe for
DMV Community President 2014 hatutambui uongozi mpya ulio tangazwa na Tume ya
Uchaguzi jana August 11, 2014. Msimamo
wetu ni kuwa; tunapinga matokeo ya uchaguzi ulio fanyika August 9, 2014 kwani
ulikuwa sio wa haki na ni BATILI.
“Team Libe for DMV Community President 2014” haitatoa
ushirikiano wowote na uongozi wa Jumuia ya Association of Tanzania Community in
DMV. Pia tunawaasa wale wapenzi wetu
kuto kutoa ushirikiano wowote na uongozi huu batili hadi pale madai yetu
yatakapo sikilizwa na kutatuliwa.
Tunaomba wapenzi wetu ambao walijitokeza kupiga kura wawe wavumilivu na
watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kunyang’anywa haki yao ya kimsingi ya
kumchagua kiongozei wanao mtaka.
Mwisho, “Team Libe for DMV Community President 2014”
inaitaka “Board of Directors” kutengua uongozi huu uliopatikana kwa njia ya
dhulma. Ieleweke kuwa, Team Libe for DMV
Community President 2014” na wafuasi wake hatutatoa ushirikiano wowote na
uongozi wote wa jumuia.
Fuata hizi link kusoma maelezo juu ya
ubatili wa huu uchaguzi;
Imetolewa August 12, 2014
Team Libe for DMV Community President
2014
No comments:
Post a Comment