Ni masaa 24 yamepita toka
uchaguzi ufanyike huku Tume ya Uchaguzi bado imekuwa na kigugumizi kutoa
msimamo na kutangaza matokeo. Uchaguzi
huu uliofanyika August 9, 2014 umedhihirika pasi na shaka kuwa ni BATILI. Baadhi ya mambo yanayofanya uchaguzi huu ni
batili na “Team Libe for DMV President 2014” inaweka wazi msimamo wake kuwa,
HATUTAKUBALI MATOKEO YEYOTE YATAKAYO TOLEWA NA TUME KWA SASA KWANI UCHAGUZI HUU
NI BATILI “FRAUD ELECTION”.
Baadhi ya sababu zinazo
batilisha uchaguzi huu ni kama zifuatazo;
Moja, jumla ya watu walio piga kura ilikuwa 430
huku Idd Sandaly alipata jumla ya kura 231 na Liberatus kura 214. Ukijumlisha kura za Liberatus na Idd unapata
kura 445, yaani kura maruhani ni 15 (214+231=445). Hii ina maanisha kuwa, Liberatus alipata
49.76% na Idd alipata 53.72% ya kura zilizo pigwa. Ukijumrisha hizi asilimia unapata 103.48%
(53.72+49.79= 103.48%). Hii ni bila
kuweka “absentee ballot. Ukiweka absentee ballot Liberatus ana kura 222 ambayo
ni 51.62% ya kura zilizo pigwa na Idd ana 235 ambayo ni 54.65% ya kura zilizo
pigwa. Hii ina maanisha ukijumrisha
jumla ya asilimia za Idd na Liberatus unapata 106.27% (51.62%+54.65%). Hii haileti maana yeyote kama wagombea wote
wana kura zaidi ya asilimi 50% ya zilizopigwa; UCHAGUZI HUU NI BATILI.
Pili, baada ya mkanganyiko huu
kutokea, wakala wa Liberatus hakuyakubali matokeo na wala hakuweka sahihi. Aliomba kura zihesabiwe tena;
alikataliwa. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi
baada ya kuona mkanganyiko huu alitamka kuwa uchaguzi huu ni “VOID” na hawezi
kumtangaza mshindi. Mzee Safari
alishinikizwa na baadhi ya watu wa Board of Trustee akiwepo Ulotu, baadhi ya
watu wa Tume ya Uchaguzi na mashabiki wa Idd Sandaly atangaze matokeo. Mzee Safari
alisema hatotangaza matokeo na kama mnataka kutangaza; chukueni mic hii hapa. Baada ya mtafaruku huu, Mwenyekiti wa Board of
Trustee, Hamza Mwamoyo, alimuita Mzee Safari faragha. Baada ya Mzee Safari
kurudi alisema “sitatangaza mshindi bali nitatangaza numbers”. Hadi leo hii
Jumapil, August 10, 2014, 9pm hakuna mshindi aliyetangazwa wala Tume haijatoa neno.
UCHAGUZI HUU NI BATILI.
Tatu, mwenyekiti wa Board of
Trustee, Hamza Mwamoyo, alizichukua kura zote akimuahidi wakala wa Liberatus
kuwa tutafanya “re-count” na akamuagiza amwambie Liberatus anipigie simu ili
tuone tutafanya vipi “re-count”.
Liberatus alimpigia simu Hamza Mwamoyo zaidi ya mara tano bila majibu. Mzee Mwamoyo alitokomea na kura zile kusiko
julikana. Hadi walaka huu unaandikwa
baada ya masaa 24; Ndg Hamza Mwamoyo hajarejesha simu ya Liberatus. Swali la kimsingi ni kuwa; inakuaje kura za
makatibu zilifanyiwa “re-count” na gap yake ilikuwa kubwa kuliko kura za marais
na za marais zikataliwe kufanyiwa re-count? UCHAGUZI HUU NI BATILI
Nne, watu waliopiga kura walikuwa 430, kura za
makamu wa Rais zilikuwa kama ifuatavyo; Heriet Shangarai kura 333 na mama Salma
Moshi kura 94. Ukijumrisha hizi kura unapata jumla ya 427 (333+94). Matokeo haya bado yapo chini ya jumla ya watu
waliopiga kura 430 (let say kura 3 ziliharibika). Wakati kura za maraisi jumla yake ilikuwa 445;
je kura 15 zilitokea wapi? Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi, Asha Nyang’anyi, amekili
kuwa kuna kura ziliharibika na wala hakusema ni ngapi. Alisema nyingi. Baada ya kumbana sana aliendelea kusema
nyingi bila kuwa “specific” ni kura ngapi ziliharibika. Hata kama kuna kura nyingi zilizo haribika;
bado zitakuwa zinaenda nje ya kura halali 430.
Kura za katibu zilikuwa kama
ifuatavyo; Said Mwamende alipata kura 251 na Ismail Mwilima alipata kura 171. Ukijumrisha kura hizi unapata jumla ya 422
(251+171). Bado kura za makatibu zipo chini ya jumla ya wapiga kura walio tokea
430; hii inamaana kura 8 ziliharibika. Je,
ni kwa nini za marais zilizidi kura 430 hadi kufikia kura 445? Kura 15
zilitokea wapi?. Makamu wa katibu
Bernadeta Kaiza alipata kura 254 na Solomn Cris alipata kura 167; jumla ya kura
hizi ni 421 (254+167). Bado na hizi zipo
chini ya jumla ya watu walio kuja 430; hii inamaana kura 9 ziliharibika. Kwa
nini za maraisi zinazidi watu walio kuja?
UCHAGUZI HUU NI BATILI
Tano, Ndg. Idd Sandaly amekuwa
akijitangaza kuwa yeye ni mshindi na leo hii jumapili August 10, 2014 alikuwa
kwenye mkutano wa CCM akijitangaza kuwa yeye ni Rais wa DMV. Je, Idd amejuaje kuwa yeye ni Rais mpya wa DMV
ilihali Tume bado haijatangaza mshindi?
Kwa hoja hizi tajwa “Team Libe
for DMV Community President 2014” inapenda kuchukua fursa hii kuutangazia Umma
wa DMV na wapenzi wake 222 yaani 51.62% ya wapiga kura kuwa: HATUTA
TAMBUA MATOKEO YEYOTE YATAKAYO TANGAZWA NA TUME JUU YA UCHAGUZI HUU BATILI. “Team Libe for DMV Community President 2014”
bado inaamini Board na Tume ya Uchaguzi watatumia busara kutatua mgogoro huu
ili tuwe na jumuia isiyo na mpasuko. Pia, wahusika watambue kuwa; Team
Libe ina watu zaidi ya 222 (51.6% ya walio piga kura 430) ambao wanahitaji
kupewa majibu stahiki. Ustawi wa jumuia upo mikonpni mwa Tume ya
Uchaguzi. Nawahasa watu wa Team Libe for DMV president wawe na
uvumilivu huku tukisubiri kauli ya Tume ya Uchaguzi.
Imetolewa August 10, 2014
Mwanaid Love “Mona”/
Campaign Manager
UNITED WE STAND; DIVIDED WE
FALL
No comments:
Post a Comment