Friday, August 22, 2014

WACHENI PROPAGANDA KWENYE MASWALA YA MSIBA YA WATANZANIA MAREKANI. UCHAGUZI WA DMV 2014 NI BATILI

Ni kwa masikitiko makubwa sana Team Libe inatoa tamko la kulaani kitendo cha Team Idd na Vijimambo Blog kufanyia propaganda picha ya msibani Cleveland ya Bwn Alawi Omar na Idd Sandaly kwa Kuweka heading ya kizushi " HUU NI MFANO WA KUIGWA" kwenye picha hiyo ya msiba ambao watanzania walikutana kwenye maziko ya kumpoteza mtanzania mwenzetu. Huu ulikuwa msiba binafsi (Private matters) ambao hauhusiki na maswala ya jumuia ya DMV na yaliojiri. Team Libe inaomba ifahamike kwamba wale wote walio jihusisha kwenye propaganda hii inaomba  watambue kuwa; msiba huwa hautaniwi wala haufanyiwi siasa.  Ni fedheha, dhihaka na dharau kwa ndugu wa marehemu kutumia msiba kwa ajili ya kujipatia maslahi binafsi(Kiki) pia kutaka  kuhalalisha uchaguzi usio halali.

Team Libe inaomba picha hiyo iachwe kutumika MARA MOJA  na WAHUSIKA WOTE WAOMBE RADHI MARA MOJA  kwa familia ya marehemu na jumiya kwa ujumla.

Tunaomba itambulike kuwa, msimamo wa “Team Libe for DMV Community President 2014” upo palepale; hatutambui uongozi mpya ulio tangazwa na tume ya uchaguzi August 11, 2014.  Msimamo wetu ni kuwa; tunapinga matokeo ya uchaguzi ulio fanyika August 9, 2014 kwani ulikuwa sio wa haki wala huru; ni uchaguzi BATILI.

“Team Libe for DMV Community President 2014” haitatoa ushirikiano wowote na uongozi wa Jumuia ya Association of Tanzania Community in DMV.

Kwa maelezo juu ya tamko la kupinga uchaguzi huu fuata link hii hapa UCHAGUZI WA DMV NI BATILI

Imetolewa August 22, 2014
Alawi Omar

Team Libe for DMV Community President 2014/ Campaign Strategist.

No comments: