-Awapotosha
waTanzania ili wasije kuongea na Rais Kikwete
-Amdanganya Rais
Kikwete darasa la Kiswahili lipo “Summer Break”
-Mh. Kikwete
amwambia Idd Sandaly “YOU ARE ON YOUR OWN”
“Team Libe for
DMV Community President 2014” inatoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzaniza Mh. Jakakya Mrisho Kikwete kwa kutumia muda wake wa
thamani na kukutana na waTanzania hapa DMV. Zaidi, tunapenda kutoa pongezi nyingi kwa mama
Balozi Liberata Mulamula na wafanyakazi wa ubalozi kwa kuonyesha ushirikiano
mzuri na watanzania wa hapa Marekani siku ya jana Jumamosi August 2, 2014. “Team Libe for DMV Communoty President 2014”
tunasema asante!
Baada ya kumaliza
kutoa shukrani za dhati kwa Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi, Liberatus Mulamula; “Team Libe for DMV Community 2014” tunaamini kuwa tuna wajibu wa
kutoa mrejesho juu ya kilichojili kwenye mkutano na Rais. Tutaanza kutoa mrejesho juu ya upotoshaji
uliotawala kwenye zoezi zima la kuongea na Mh. Rais. Zoezi hili liliongozwa na Rais wa DMV aliye
maliza muda wake Ndg. Idd Sandaly kwa kufanya upotoshaji ufuatao;
Upostoshaji wa kwanza ulio fanywa na Idd Sandaly ni kuwa; watu
wote walio taka kuja kuongea/kumuona Rais, Jakaya Kikwete, iliwapasa waje na ID
au Passport. Upotoshaji huu ulikuwa
umewekwa ili kuwawanyima haki waTanzania wasio na ID au wametokea kupoteza
passport kwa bahati mbaya. Ukweli ni kuwa; kwenye kumuona Mh. Rais kulikuwa
hakuna maswala ya kuonyesha ID wala passport. Watu waliingia bila kuonyesha hivyo
vitambulisho.
Upotoshaji wa pili ulio fanywa na Ndg. Idd Sandaly ili
awezi kuwanyima waTanznia haki ya kukutana na Rais wetu ni kuwa; Idd alitoa maelekezo
kuwa mkutano na Rais utaanza saa 12 jioni (6pm) na watu wanatakiwa kuwa pale saa
11:40 (5:40pm) na endapo usipo kuwapo pale kwenye huu muda, hautaruhusiwa
kuingia. Ukweli ni kuwa, mkutano ulianza
saa 1:30’s (7:30’s pm), na watu walikuwa wanaingia muda wowote. Huu upotoshaji umewasababishia watu wengi
kuto kuja au kupoteza masaa yao ya kazi na shughuri zingine.
Upotoshaji mwingine ulio fanywa na Idd Sandaly ni kuwa;
alikuwa akitoa taarifa kuwa watu wanao takiwa kuingia ni 250 na hakuna mtu
atakaye ongezwa kwenye “roaster” endapo asipo rudisha jina lake kabla ya Ijumaa
saa sita mchana. Ukweli ni kuwa; kulikuwa na watu zaidi ya 300 na wengine
walikosa viti. Sio hilo tu, wapo wale
ambao waliandikishwa baada ya saa sita mchana Ijumaa, kitu ambacho si haki kwa
wale walio tiwa upofu na upotoshaji huu. Huu upotoshaji unatukumbusha kilicho
tokea December 2013 “Uhuru Day” ambapo Idd Sandaly akishirikiana na Vijimambo
blog aliweza kuwa “rip off” wana DMV $60.00 na kuwapeleka kwenye Godauni ambalo
lilikuwa na vumbi, hakukuwa na security, na pombe ilitolewa mbele ya watoto. Hii ilikuwa siku ambayo Mh.January Makamba
alikuja DMV.
Upotoshaji mwingine wa Idd Sandaly ni kuwa alitumia mkutano
wa Mh. Rais Jakaya Kikwete na waTanzania kama sehemu ya kufanyia kampeni. Hii
ilidhihirika pale ambapo Idd Sandaly alipo jipigia debe mbbele ya kadamnasi na
kusema “uchaguzi Jumamosi naomba mnipigie kura”. Busara za Mheshimiwa Kikwete
zilitamaraki na kumjibu kwa nkumruka akasema “ YOU ARE ON YOUR OWN”.
Upotoshaji wa mwisho ambao ni hatari kwa taifa ni Idd Sandaly
kuongea UONGO mbele ya Rais. Ndg Idd Sandaly amemdaganya Mh. Rais Jakaya
Kikweti, balozi Liberata Mulamula, Waziri Bernad Membe, waziri Magufuli, naibu
waziri wa nishati Mh. Stephene Masele na waTanzaia wote walio kuwepo kwenye
mkutano na Rais jana kuwa DARASA LA KISWAHILI LIPO na watoto wapo “Summer
BREAK”. Huu ni UONGO ambao unaonyesha
Idd Sandly ni kiongozi wa aina gani kwa kuwadanganya watanzania na Mh. Rais
Jakaya Kikwete. Kiongozi anaye danganya
umma hana maadili wala dhamana ya kuongoza.
UONGO wa Idd Sandaly kuwa darasa la Kiswahili lipo “Summer break” unathibitika
kwa sababu zifuatazo: Mosi, hakuweza kusema hiyo “Summer Break” itaisha lini
(ni ya muda gani), pili hakuweza kutoa anuani ya darasa (darasa lipo wapi) na
tatu darasa lime kufa kabla ya February 2014; hatuna uhakika kama “Summer
Break” ya darasa hili huanza February!
Mwanaid
Love “Mona”
Campaign
Manager
Team
Libe for DMV Community President 2014
1 comment:
Iddi ni Mfa maji
Post a Comment