Baada ya muda wa ukumbi kuisha na kura zikiendelea kuhesabiwa:
matokeo yalikuwa kama ifuatavyo;
Urais
Idd Sandaly kura 231
Liberatus Mwangombe Kura 214
Jumla ya watu walio piga kura ilikuwa 430
Hii inamaanisha Idd amepata 53.7% ya kura zilizo pigwa na Liberatus amepata 49.76% ya kura zilizo pigwa. Ukijumrisha hizi asilimia, unapata 107.89%. Swali; 7.89% imetoka wapi?
Ukijumlisha kura za Idd na Liberatus 231 +214= 445. Hii inaonyesha tofauti ya kura 15 huku Idd
akiongoza kwa kura 17. Hii inamaanisha
kulikuwa na kura za ziada 15, yani kura 15 zilikuwa hazijulikani zilipo
toka.
Wakala wa Liberatus alipewa kura 8 za absentee ballots na
wakala wa Idd alipewa kura 4 za absentee ballots. Tatizo hapa; hatukupewa idada ya watu walio
piga absentee ballot na wala hawakusema ni ngapi zimeharibika.
Ukijumrisha kura za ukumbini na absent ballot, matokeao ni;
Idd Sandally 231+4= 235
Liberatus Mwangombe 214+8= 222
Hii inaonyesha Idd anaongoza kwa kura 14
Swali kuu ni kuwa; Zile kura 15 zilizo zidi zime tokea wapi?
Baada ya kuona mapungufu haya kwenye kura; Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi Ndg. Safari alitamka kuwa uchaguzi huu ni “VOID” na hawezi
kutangaza mshindi; lakini atatangaza numbers. ALITANGAZA NUMBERS ZA UWANJANI
TU, HAKUTANGAZA ABSENT BALLOT. Wakati sintofahamu
hili likienedelea; “Team Libe for DMV Community President” iliomba “re-count”;
ikashindikana kufanya re-count baada ya polis kuchukua mic na kufukuza kila mtu
ukumbini. Watu wote walitoka ukumbini
ndani ya dakika moja. Ikumbukwe; ukumbi ulichukuliwa
hadi saa nne usiku. Wakati tunafukuzwa
na polis ilikuwa ni saa tano usiku. Mwenyekiti
wa Board Ndg. Hamza Mwamoyo aliondoka na kura zote akidai tutafanya re-count.
Kipengele kingine ambacho kilikuwa na utata ni cha makamu wa Rais. Ieleweke kuwa; box la makamo wa rais na Rais lilikuwa moja.
Nafasi ya makamu wa Rais matokeo yalikuwa kama ifuatavyo;
Heriet Shangarai kura 333
Salma Moshi kura 94
Ukijumrisha matokeo ya makamu wa raisi unapata jumla ya kura
429. Hii bado inaonyesha ukakasi; kwa
nini kura za Rais ziwe jumla 445 na makamu 429 na zote zimetoka kwenye box moja;
na karatasi linalo tumika kupigia kura lina katwa sehemu mbili, ya juu ni ya Rais
na chini ya Makamu wa rais; zote zinaingia kwenye box moja. Hoja; kwa nini number za makamu wa Rais na
Rais don’t add up! Au, kwa nini number za mgombea wa makamu wa mwenyekiti zime “match” na wapiga kura; wakati number za
raisi hazijamach na zote zinatokea wenye box moja (zinatofauti ya kura 16)?
Itambulike kuwa; msimamo wa “Team Libe for DMV Community
President 2014” unaamini Board na Tume ya Uchaguzi watatumia busara kutatua
mgogoro huu ili tuwe na jumuia isiyo na mpasuko. Pia, wahusika watambue kuwa; Liberatus ana watu
zaidi ya 222 (51.6% ya walio piga kura 430) ambayo ni walio mpigia kura ambao wanahitaji
kupewa majibu stahiki. Ustawi wa jumuia
upo mikonpni mwa Tume ya Uchaguzi. Nawahasa watu wa Team Libe for DMV president
wawe na uvumilivu huku tukisubiri kauli ya Tume ya Uchaguzi.
Imetolewa August 9, 2014
Mwanaid Love “Mona”/ Campaign Manager
UNITED WE STAND; DIVIDED WE FALL
No comments:
Post a Comment