Naitwa Dr Allan,MD., MPH. Naipenda Jumuia yetu ya DMV na napenda sana kuona mabadiliko chanya katika mambo mbali mbali yanayotuhusu na yanayoihusu Jumuia yetu. Kwa sasa nipo Tanzania, Kura yangu through absentee ballot (procedures zote zimeshafuatwa) imeenda kwa Liberatus MwangOmbe(urais) na Solomon(Katibu msaidizi), Hawa sii tu kwamba ni watu ninaowafahamu na tuliobahatika kwenda same high school (Tambaza) japo kwa vipindi tofauti-BALI wameweza kujipambanua kwa ufasaha na kwa kutumia simple and clear non abusive language kujenga hoja makini na zenye MASHIKO katika kutengeneza sera na miongozo tarajiwa-katika kuipeleka jumuia yetu to the "next level".
Kikubwa ambacho hatuhitaji chaki au daftari na kalamu kueleweshwa ni INCLUSIVE INVOLVEMENT/PARTICIPATION OF EVERY COMMUNITY MEMBER katika kila jambo linalotuhusu kama Jumuia, hii nia dhahiri ya UWAZI ni alama tosha ya nia njema kwa jamii na Jumuia yetu, kitu ambacho Jumuia yetu kwa miaka mingi tulikikosa na kusababisha kupoteza imani kwa Viongozi wa Jumuia, na Jumuia kwa ujumla-kwa watanzania wengi wa DMV.
Shime wana DMV, SOLUTION YA KUUJENGA UPYA NA KUUIMARISHA UPYA UMOJA WETU NI "LIBE+His Cabinet" PEKEE! Hivyo basi, Wakati wa mageuzi ni sasa, naomba tuwape support na tujitokeze kuwapigia kura watu hawa ili tusonge mbele kwa ustawi BORA wa sasa na wa baadae wa Jumuia yetu.
VOTE FOR LIBE AND SOLOMON FOR POSITIVE INNOVATIVE CHANGE!!
No comments:
Post a Comment