Thursday, July 31, 2014

UCHAGUZI DMV USA: IDD SANDALY NA MRADI MFU WA VITABU ULIO IGHARIMU JUMUIA $1200.00

Na Faustus

       Ndugu Idd Sandaly inakubidi uache kulialia na uwe mkweli kwenye Jumuia yetu. Mimi Faustus mkazi wa DMV nimechoshwa na uongo unao utoa kwenye “social media” wa kujigamba kuwa umekusanya vitabu kwaajili ya nyumbani Tanzania. Idd, kwa nini unaongea UONGO, ilihari unajua kuwa “MRADI WA VITABU” ni MFU? Ndg. Idd Sandaly umekuwa ukiuelezea Umma wa DMV na duniani kote kwa kujinasbisha na picha za vitabu kuwa mradi huo ni wa mafanikio. Muogope mungu kaka! Unajua wazi kuwa mradi huo wa vitabu ni mfu na umeisababishia jumuia hasara ya $1200.00.

Mradi huu wa vitabu ambao Ndg. Idd Sandaly unautumia kwa kampeni haujailetea manufaa yeyote jumuia yetu, bali hasara ya “storage fee” ya $1200.00.  Ukweli ni kuwa ulikusanya vitabu hivi ili upige picha bila kujua ulilokuwa unalifanya. Matokeo yake imethibitika pasi na shaka kuwa hivi vitabu haviendani na mitaala ya Tanzania. Kwa hivi sasa baada ya mradi huu mfu wa vitabu kuitia hasara jumuia ya $1200.00 (storage fees) inafanyika mipango ya kuvitupa.
Huu ndio mradi wa vitabu ambao Ndg. Idd Sandaly anajinasbisha nao kwa picha.UKWELI; mradi huu umeipa hasara jumuia ya $1200.00 na sasa vinataka kutupwa

Ukweli mwingine unao umiza ni kuwa (source; kutoka ndani ya uongozi wa jumuia), “All Afrika Logistic” ilijitolea kusafirisha vitabu hivi hadi Tanzania bure. Zaidi, vitabu huwa havilipiwi kodi. Cha ajabu ni kuwa Idd Sandaly ulikataa kutumia fursa hii na kuendelea kuviweka vitabu hivi “storage” ambapo vime iingizia gharama jumuia ya $1200.00. Kilicho nyuma ya pazia kuendelea kuweka vitabu hivi storage ni kuwa; Idd Sandaly umekuwa ukisafirisha mizigo Africa; kabla ya kusafirisha mizigo yako umekuwa ukiihifadhi storage na hivyo vitabu na kupeleka “bills” kwa jumuia. Maswali ya kujiuliza ni yafuatayo;

  • ·   Je, Vitabu hivyo vilikuwa vingapi na vilikuwa na ukubwa gani hadi viigharimu jumuia $1200.00
  • ·  Pili, vitabu hivyo vilikaa “storage” muda gani hadi viigharimu jumuia $1200.00

Itakuwa ni busara kwa Ndg. Idd Sandaly kuuelezea Umma wa DMV kwa nini unatumia mradi huu MFU kwenye kampeni; huku ukitambua wazi kuwa mradi huu umefeli. Hii inadhihirisha usanii kama ulio ufanya kwenye insha ya maneno zaidi ya 580 ukielezea kuwepo kwa darasa la Kiswahili; huku ukishindwa kueleza lipo wapi (address) au kuwa specific na tarehe ya kurudi.

Faustus




1 comment:

Anonymous said...

Hahaha!!!!