Wednesday, July 23, 2014

OFFICIAL STATEMENT: JUU YA MREJESHO WA KIKAO NA BALOZI LIBERATA MULAMULA

Na Liberatus Mwang’ombe

July 23, 2014


REF: UCHAGUZI DMV: MREJESHO WA KIKAO CHA WAGOMBEA NA BALOZI MULAMULA WA July 19, 2014

Napenda kuchukua fursa hii kuweka jambo moja sawia kuhusu mrejesho wangu juu ya kikao na mama balozi Liberata Mulamula.  Kumekuwa na upotoshaji kuwa mrejesho wangu ulilenga kumvunjia heshima Mh. Balozi Mulamula, LA HASHA! Mrejesho ule ulilenga kuwaeleza wana DMV  UWAZI na UKWELI juu ya kilicho jiri kwenye mkutano kwani wao ndio walio omba Balozi aitishe Suluhu.  Inawezekana kuna maneno yalitumika ndivyo sivyo kwenye walaka ule kutokana na mtazamo wa msomaji; naomba Umma utambue kuwa, lengo langu halikuwa kumkwaza Balozi wetu.

Pili  kilicho sahihi kwako au kwangu kinaweza kutafsiriwa vingine na mwingine.  Hivyo basi, kama kuna sehemu yeyote ya ule walaka ambapo "Team Libe for DMV President 2014"  ilitoa ukatafsiriwa ndivyo sivyo ; Tunaomba ieleweke  kuwa, Balozi Mulamula hakuwa mlengwa na tuna omba radhi kwa hilo.

Pia,  Umma wa DMV na duniani kote tunaomba mtambue kuwa; nina muheshimu mama Balozi Mulamula kama muwakilishi wa nchi yetu, Tanzania, hapa USA na nina muheshimu kama mama yangu. Naomba Umma wa DMV utambue kuwa, mimi, Liberatus Mwangombe, sitajihusisha kwenye kampeni za kubomoa wala kejeli kama inavyo tafsiriwa na Upinzani. Kampeni zangu zitajikita kwenye hoja na agenda juu ya nini kama wana DMV tukifanye ili jumuia yetu iwe ni Jumuia inayo waunganisha waTanzania na kuwapa matumaini ya kufanya wajikwamue kiuchumi, kijamii na kuifanya DMV kuwa sehemu bora zaidi ya kuishi. Mwisho, nafunga mjadala huu na sintakuwa tayari kuendeleza majibishano kuhusu huu mjadala.

Asanteni!

UNITED WE STAND; DIVIDED WE FALL
UNITED WE STAND; DIVIDED WE FALL

No comments: