Tumesikitishwa
na upotoshaji ulio fanywa na Ndg. Adam Tenga juu ya wanao msupport mgombea wa
Urais DMV, Liberatus Mwangombe, kuwa wana chuki binafsi na Ndg. Idd Sandaly. Ngd. Tenga kwa kutumia blog ya Vijimambo
ametoa shutuma nzito, zisizo na ushahidi na za uongo dhidi ya wanao muunga
mkono Ndg. Liberatus Mwangombe “Libe” kuwa sababu yao kuu ni kuwa na maswala
binafsi na Ndg Idd Sandaly. Huu ni uongo
na upotoshaji unao toka kwa mtu asiye jitambua wala kujua jinsi hii dunia
inavyo jiendesha kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Kitendo
cha Ndg. Tenga kusema “WATU WOTE WANAO
MSUPPORT ‘LIBERATUS’ WANA CHUKI BINAFSI NA IDD” kinaonyesha ufinyu wa fikra
kwa msingi kuwa; yeye (Adamu) hajaongea
na watu wote wanao msupport Ndg. Liberatus na kujua kwa nini wameamua kuachana
na Idd na kumsupport Liberatus. Kauli ya
Adamu Tenga inaonyesha ni kiasi gani anataka kupandikiza chuki kati ya wana
DMV; kwani ametoa kauli hii bila kuwa na ushahidi wala ukweli wowote. Kama ana
ushahidi, athibitishe. Kauli hii ni
kejeli na dharau kwa wana DMV. Kwa kauli
hii, Adamu Tenga ameweza kuthibitisha kuwa Idd Sandaly ana matatizo binafsi na
watu wengi hapa DMV; sio sifa nzuri kwa kiongozi (hii ni tafsiri isiyo rasmi ya
maneno ya Adamu Tenga).
Team
Libe for DMC Community President 2014 tunapenda kuujurisha Umma wa DMV na
duniani kote kuwa waangalifu na wapotoshaji kama Adamu Tenga. Team Libe for DMV
President 2014 tunatambua na kuamini kuwa huu uchaguzi unahusu tofauti/ushindani
wa kisera/agenda na sio tofauti/ushindani binafsi (chuki binafsi).
TEAM LIBE FOR DMV
PRESIDENT 2014 BELIEVES IN CONFLICT OF IDEAS; NOT CONFLICT OF PERSONALITIES
UNITED WE STAND; DIVIDED WE FALL
Imetolewa na Mwanaid Love “Mona”
Kampeni Manager
Kampeni Manager
July 13, 2014
Team Libe for DMV Community President 2014
2 comments:
Libe kafulia aende akalime siasa au uongozi kaujulia wapi
mimi sikujuwa kama darasa la kiswahili limekufa kwa miezi 6 why?
Pili walimu wa darasa la kiswahili wako 4 or 6 nadhani sasa Asha wewe kila likizungumzwa darasa la kiswahili lazima umtete idd ,jasho linakutoka kwani mwalimu ulikuwa peke yako? Kwenye darasa hilo? Mbona wengine hawajibu ndio kusema hawakubaliani na mr idd asemavyo?? Au wewe asha una uhusiano na mr sandaly zaidi ya huu tunaojuwa kuwa ni volunteer? Tu?
Huweleweki mtu mzima wewe.
Post a Comment