Na Liberatus Mwang’ombe "Libe"
Nikiwa kama mwana Diaspora nimekuwa nikifuatilia maendeleo ya
mchakato wa kupata katiba mpya nyumbani.
Kama mTanzania ninaye jishirikisha na mambo ya nyumbani kwa karibu;
nimeweza kuiandikia Tume ya Katiba maoni kwa ajili ya kupata katiba mpya
likiwemo swala la “URAI PACHA”. Kwenye
insha hii nitaelezea jinsi nilivyo sukuma uraia pacha kwa jitihada
binafsi. Pia nitaweka link na picha ya
“petition” niliyo ianzisha kipindi cha kukusanya maoni ya katiba. Petition hii iliweza kusainiwa na waTanzaina
90; idadi ambayo ni kubwa kuliko maoni yaliyo tolewa na waTanznia wote kwenye
tume ya katiba juu ya uraia pacha.
Hii ndio sura ya "petition" ya uraia pacha niliyo ianzisha August 2013
Petition hii ya maoni kwa tume ya katiba niliianzisha August
26, 2013 kwa lengo la kuongeza msukumo wa uraia pacha kwenye tume ya katiba. Kwa kila mTanzania aliye weka sahihi alipata
“confirmation” kwenye barua pepe na barua pepe nyingine ilitumwa kwenye Tume ya
Katiba moja kwa moja. Baada ya tume ya
katiba kumaliza muda wa kuchukua maoni; nili iunganisha petition hii na email
za wabunge wa Bunge la jamuhuri ya Muungano ili mTanzania akiweka sahihi na wao
wapate taarifa ya kilio chetu.
Sio haya tu; petition hii ili unganishwa na “email” ya Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, ili naye awe anapata
kusikia kilio cha watanzania tuliopo nje ya nchi. Kilio hiki kilisikika na wizara yake iliweza kupendekeza uraia pacha kwenye maoni yake. Maoni ya wizara yake yalikuwa kama ifuatavyo
kwenye kipengele cha 3;
3) Kuhusu suala la uraia katika Jamhuri ya Muungano;
Baraza lilipendekeza kuwa suala la uraia wa nchi mbili kwa Mtanzania wa
kuzaliwa litamkwe Kikatiba na Raia huyo asipoteze uraia wake wa kuzaliwa kwa
sababu ya kupata uraia wa nchi nyingine. Uraia wa nchi mbili utatoa fursa kwa Taifa
letu kufaidika kimaendeleo kutokana na kutumia rasilimali za Watanzania walioko
nje ya nchi;
Jitihada hizi binafsi na waTanzania wengine walio saidia
kuweka sahihi kwenye petition hii ziliongeza msukumo wa URAIA PACHA ambapo
kwenye rasimu ya pili iliyo toka November 2013, kipengele hiki kilipitishwa na
sasa kitajadiliwa Bungeni.
Petition hii bado ipo wazi na unaweza kuweka sahihi ili tuendelee kuweka mkazo kwa wabunge wa Bunge Maalumu la katiba BONYEZA HAPA KUWEKA SAHIHI PETITION HII
Mchango wangu haukuishia hapo bali uliendelea; mnamo November
30, 2013 nikiwa kwenye Miss Tanzania USA Pageant na Mbunge Leticia Nyerere
nilimkutanisha Rais, Idd Sandaly, Makamu wake, Raymond Abraham, na Mbunge huyu nikiwa
na wazo la kuwaomba tutafute watu ili waende Dodoma kipindi cha Bunge la Katiba
kwaajili ya "Lobbying". Mbunge Nyerere aliahidi kutoa
ushirikiano pindi wana Diaspora wataenda Dodoma. Zaidi ya haya; nilitoa wazo la
kuanzisha petition kama jumuia kwaajili ya swala hili. Mawazo haya yalipokelewa
na uongozi wa jumuia na kutendewa haki. Kwa sasa petition inayo endelezwa na
jumuia ina sahihi zaidi ya 1700 na sahihi yangu ikiwa ya mwanzoni na
"nilishare" hii petition kwenye social media. Zaidi, mchango wangu wa fedha za lobbying ulikuwa $200.00 ili kuhakikisha tunapata uraia pacha.
Yafuatayo ni maoni ambayo nilituma moja kwa moja kwenye tume ya katiba pembeni ya petition niliyo anzisha
January 16, 2013
To: Tume ya Mabadiliko ya Katiba
From: Liberatus Mwangombe
Re: Mchango wangu wa KATIBA mpya
Moja: Uwazi wa mishahara ya wanasiasa
Katiba mpya iruhusu kuweka wazi mishahara ya wana siasa na
marupu rupu yao (pamoja na Rais). Viongozi wa nchi ni waajiliwa wa wananchi,
hivyo basi ni haki ya muajili kujua anamlipa muajiliwa wake kiasi gani.
Pili: Adhabu ya kifo
ADHABU YA KIFO ifutwe. Kwa jinsi dunia inavyoendelea
kisayansi na technologia kuna uwezokano mkubwa mtu kuonekana na hatia leo na
kuhukumia kifo na miaka ijayo kuzihilika kuwa alikua hana hatia. Mfano, mtu huyo
ananyongwa baada ya kukutwa na hatia. Baada ya miaka kumi (kunyongwa) kutokana
na kukua kwa sayansi na technolojia inagundulika kuwa mtu aliye nyongwa hakua
na hatia. Tutawezaje kumrudisha? Tumeona mifano mingi kwenye nchi zilizo
endelea, watu wapo kwenye “death row” lakini DNA imekuja kuwatoa kwenye hatia
baada ya miaka mingi kwa ajili ya kukua kwa sayansi na technologia.
Tatu: Umri wa kugombea nafasi
Umri wa kugombea nafasi za uongozi ushushwe (pamoja na
Uraisi). Kama mtu wa miaka 18 au 21 anaweza kuchagua kiongozi, kutumika jeshi
au polisi, ni haki kuwa na HAKI ya kuchaguliwa kutumikia ofisi yoyote ya
serikali.
Nne: Urai pacha
Kwa jinsi dunia inavyo badilika, sasa ni muhimu kuruhusu
uraia pacha. Tanzania tupo katika nchi za Africa mashariki, Kenya na Uganda.
Wenzetu hawa wamesha ruhusu uraia wa nchi mbili, hii inawapa nafazi zaidi kuwa
washindani katika level ya kimataifa kuliko sisi. Tunahitaji hili ili tuweze
kuwa na nafasi sawa na wenzetu wa Afrika mashariki na dunia kwa ujumla.
Tunaweza kutengeneza misingi kwenye katiba yetu ambayo itakuwa vigumu kwa
wageni kuchukua uraia wa nchi yetu. Mfano, mtu hawezi kuwa raia wa Tanzania
hadi awe ameishi Tanzania kwa miaka ishirini na asiwe amevunja sharia yeyote ya
nchi. Pili, mtu anaweza kuvuliwa uraia kama atavunja sharia za nchi. Au,
tunaweza kuweka sharia ya kuto toa urai kwa wageni na Mtanzania yeyote mwenye
uraia wa nchi nyingine akiwa Tanzania ni lazima afuate sharia za nchi hadi pale
atakapo toka nje ya mipaka na atachukuliwa ni mtanzania wa KUZALIWA. Kumbuka,
waTanzania wanao chukua raia nyingine ni waTanzania wa kuzaliwa, mioyo yao ni
Tanzania, majina yao ni Tanzania, ndugu zao ni waTanzania, wanaipenda Tanzania,
na wanazungumza Kiswahili, isipo kuwa sio waTanzania kwenye makaratasi. Achilia
mbali mchango wao kwa Taifa.
Tano: Viti maalumu
Viti maalumu viondelewe kwenye katiba. Viongozi wanapaswa
kuwawakirisha wananchi, hivyo basi inapotokewa kiongozi anateuliwa na Raisi
anakuwa ana kila sababu ya kutetea maslai ya aliye mteua (Raisi) badala ya
wananchi.
Sita: Madaraka ya raisi
Raisi asiruhusiwe kuchagua wakuu wa mikoa bali apewe madaraka
ya kuchagua baraza lake la mawaziri ambalo wachaguliwa wasiwe wabunge. Pia,
wakuu wa mikoa wachaguliwe na wananchi badala ya kuteuliwa na Raisi.
Napendekeza kipindi cha ukuu wa mkoa kiwe cha miaka sita, lakini unaweza
kutumikia vipindi visivyo na ukomo kama ukiwa unachaguliwa kila mara.
Saba: Rasilimali
Rasilimali za madini, mafuta gesi n.k ni mali ya waTanzania.
Hivyo basi, serikali kabla ya kusaini mkataba wowote ni lazime upitiwe na
bunge.
Nane: Mamamlaka ya Bunge
Bunge kama mwakilishi wa wananchi liwe na HAKI ya
kumuwajibisha au kumfukuza kazi Raisi endapo atatumia madaraka yake vibaya. Pia
Raisi asiwe na kinga zidi ya sharia akiwa madarakani au baada ya kumaliza
uongozi.
Tisa: Elimu na Afya
Elimu na Afya iwe ni haki. Katiba iidhinishe kuwa ni HAKI kwa
kila mtanzania kupata matibabu anavyo kuwa mgonjwa na pia ni haki kwa kila
mtanzania kupata elimu. Matibabu na elimu visiwe bidhaa au biashara. Hivi viwe
basic “ HUMAN RIGHT” kama haki ya KUISHI.
Katiba ya sasa hii hapa: Katiba ya Tanzania
Liberatus Mwangombe.
240-423-3331
Kwa habari za kampeni zangu BONYEZA HAPA
WANA DMV NAOMBA KURA NA FURSA YENU YA KUIONGOZA JUMUIA
No comments:
Post a Comment