Tuesday, July 29, 2014

SERA ZA MGOMBEA URAIS WA DMV COMMUNITY LIBERATUS MWANGOMBE “LIBE”


LIBERATUS "Libe" MWANG’OMBE, MPH, BSRC, RRT-NPS.
Intern:The Division of Health Interview Statistics (DHIS) at the National Center for Health Statistics (NCHS)/United States  Center for Disease Control and Prevention (CDC)


Ushirikiano na Umoja
  •  Uongozi huu utaimarisha ushirikiano  na ubalozi wetu pamoja na wizara ya mambo ya nje, ili kupendekeza “Diaspora policy” itakayowapatia wanaDispora nafasi za kazi, mikopo nchini Tanzania na kuwezesha uraia pacha.
  • Pia tutahakikisha waTanzania  wanapatiwa fursa ya kuongea na viongozi wa serikali wakiwa kwenye ziara hapa USA, ili kujadili mambo mbali mbali  yanayoendelea nchini.
  • Mapendekezo ya  kurekebishwa kwa katiba yatafanyika awali,  ili kulinda haki za wapiga kura DMV  (Kupiga kura iwe haki kwa kila mTanzania na sio "benefit", yaani sio pay-register and vote)
  • Uongozi huu utafanya maamuzi kwa kufuata katiba ili kuleta amani, umoja na mshikamano.
  • Uongozi huu utakuwa wa uwazi na ukweli. “UWAZI na UKWELI”  ni msingi wa Imani na kichocheo cha Uzalendo
  • Katika uongozi wetu kila Mtanzania atapewa heshima stahiki na haki ya kusikilizwa na kushirikishwa 
Baraza la Ushauri
  • Uongozi huu utatambua mchango wa viongozi waliopita, viongozi  wa dini  na  wazee na kuwajumuisha katika  baraza la ushauri.  

Lugha ya Kiswahili
  • Uongozi huu unatambua mchango mkubwa uliofanywa wa kuanzishwa kwa darasa la kiswahili na utafanya juhudi za kuendeleza juhudi hizo.
  •  Nia yetu ni kukuza kitengo hiki kwa kuwakaribisha watu wa mataifa mengine  kujifunza lungha yetu ya  Kiswahili   ambayo imekubalika rasmi kwenye Umoja wa Afrika
  • Uongozi huu utajihusisha na shule za sekondari pamoja na vyuo nchini  Marekani vinavyofundisha lugha ya Kiswahili kwa nia ya kuwapatia wanajuiya ajira ya walimu na ukalimani wa lugha ya kiswahili.
Jumuiya na Wajasiriamali
  • Uongozi wetu utatumia  Association of Tanzania Community (ATC) kuwadhamini wajasiriamali   kupata mikopo midogo na mikubwa ya  kufungua biashara zao.
  • Ili kuwawezesha wajasiriamali, tutaweka taratibu za kuwapatia  mafunzo  na kufwatilia maendeleo ya biashara zao. 
Elimu 
  •    Uongozi utachukuwa jukumu la kuhakikisha kuwa, Watanzania wanapata taarifa sahihi za udhamini wa elimu  wa vyuo mbalimbali na fursa nyingine kama “Young African Leaders Initiatives” (YALI), juhudi za Rais Baraka Obama kusaidia viongozi wa kesho barani Africa. Uongozi utatoa habari ya bahati nasibu “Diversity Visa Lottery” kwa Watanzania wanotafuta fursa ya kusoma na kujiendeleza hapa Marekani.

Jumuia na vyanzo vya mapato
  •  Mapato ya jumuiya yatatokana na ‘fund rising events’ tukishirikisha mataifa mbali mbali pamoja na miradi midogo katika shuhuli hizo.
  •   Kwa kutumia hadhi ya 503 (c) tutatafuta misaada kutoka mashirika makubwa na hospitali  ili kupata  vifaa kwa ajili ya hospital za nyumbani.

Jumuia na Afya

  •   Tutaanzisha “Nursing Association” kwenye jumuia  ambayo itakuwa ikitoa mafunzo.  Pia tutatafuta namna ya kupata unafuu wa Health Insurance kama kikundi ili kupunguza gharama



No comments: