Mgombea wa Urais DMV USA Ndg. Liberatus Mwangombe akiongozana na
Mbunge wa Alumeru Mashari Mh. Joshua Nassari, July 27, 2014 walipita kumpa
mkono wa pole Mchungaji M.D. Maturlu aliye mpoteza mdogo wake Focus Maturlu
kwenye kanisa la Holy Gross Lutheran Church, Greenbelt, Maryland. Mh. Nassari alipata fursa ya kutoa maneno
machache na alieleza jinsi alivyo furahishwa na nyimbo za mapambio hapo
kanisani. Pia Mh. Nassari alieleza kujisikia kama yupo nyumbani kutokana na
ukweli kuwa amekulia kenye mazingira ya Kikristu na baba yake mzazi ni
mchungaji; hali ya pale kanisani ilimkumbusha mbali na kujikuta akicheza na
kushangilia nyimbo zilizo kuwa zikiimbwa.
Wakati huo huo mgombea Urais kwenye
jumui ya DMV Ndg. Liberatus Mwangombe “Libe” alikutana na mgombea mwenza Ndg.
Idd Sandaly na kuwa na mazungumzo ya hapa na pale huku tabasamu na vicheko vya
furaha vikiwa vimetamalaki vinywani mwao. Pia alikuwepo mgombea wa makamo wa
Rais mama Salma Mushi kwenye kumpa pole Mchungaji Maturlu.
Alipo pata fursa ya kuzungumza
machache Ndg. Liberatus “Libe” kwenye hotuba yake fupi ya dakika kama nne
alimtakia mapumziko mema marehemu Focus Maturlu. Zaidi, Ndg. Liberatus “Libe”
alieleza kuwa, Ndg. Idd Sandaly ni rafiki yake, huwa wanashirikiana kwenye
mambo ya kijamii na hucheza mpira (Soccer) pamoja. Ndg. Liberatus “Libe” aliongeza
kuwa, Idd Sandaly ni kama kaka yake na anaheshimu huduma aliyo itoa kwenye
jumuia ya DMV. Pia aliweka wazi kuwa
yeye na Ndg. Idd Sandaly hawana tofauti binafsi isipo kuwa wana tofauti za kisera
na jinsi ya kuiongoza jumuia ya DMV. Zaidi
ya hayo, Ndg. Liberatus “Libe” aliwaomba wana DMV kujiandikisha na kujitokeza
kwa wingi siku ya uchaguzi ili wawe sehemu ya historia. Ndg. Liberatus “Libe” aliwahasa watu wanao
muunga mkono baada ya August 9, 2014 bila kujali matokeo waweke ushirikiano na
kiongozi mpya wa DMV; alisisitiza umoja na ushirikiano baada ya uchaguzi.
No comments:
Post a Comment