Wednesday, July 2, 2014

NEWS ALERT: JE? NINI KILICHO ZUNGUMZWA UBALOZINI NA MGOMBEA WA URAIS DMV LIBERATUS “LIBE”

        Mgombea wa kiti cha Urais DMV, Liberatus Mwang’ombe, July 1, 2014 alipata fursa ya kutembelea ubalozi wa Tanzania Washington, D. C., ambapo alilakiwa na balozi Liberata Mulamula.  Liberatus alifika ubalozini mida ya saa nne na nusu asubuhi (10:30am) kujitambulisha kama mgombea wa kiti cha Urais DMV na kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kuwashirikisha na kuwapa wana Diaspora haki ya kutambulika kikatiba, “Diaspora policy”; na kuweza kuiwezesha jamii ya DMV kwenye mambo mbalimbali.  Pia majadiliano yalilenga namna ya kuhakikisha wana Diaspora wanaweza kushirikishwa kwenye mambo ya nyumbani na kusaidia nchi yetu kuondokana na umasikini.  Zaid, mbinu na jinsi ya kudumiza amani, umoja na ushirikiano zilijadiliwa.


       Mkutano na Balozi Mulamula ukiendelea huka Ndg. Liberatus akisikiliza kwa makini
      Kwenye mazungumzo hayo Ndg. Liberatus alisisitizia kampeni zilizo safi na zenye tija.  Alionekana akisistiza kuwa kampeni hizi ziwe za hoja na sio “personalities” wala vihoja kwani mwisho wa uchaguzi ataibuka mshindi mmoja ambaye atahitaji waTanzania wote wa DMV kumuunga mkono.  Mtazamo huu chanya uliungwa mkono na Balozi Mulamula, afisa Ubalozi Switebert Mkama, Suleiman Saleh na kampeni manage Mwanaidi “Mona”.  Mh. Balozi pia alisisitiza kuwa tushindane kwa hoja na kama itakuwa kwa vihoja ata “mobilize” watu wawakatae wagombea wote.

          Zaidi, Ndg. Liberatus alimkabidhi Balozi Mulamula sera zake ambazo zilionekana kumfurahisha.  Moja ya sera za Ndg. Liberatus ni kuwa na “Diaspora Policy” ambayo itaweza kumtambua mTanzania aliye nje ya nchi kikatiba.  Sera hii ilionekana kuungwa mkono na Mh. Balozi Mulamula huku akikiri kuwa kunajitihada za kutaka “Diaspora” yetu ijulikane na “USA machinery” ili wawekezaji wa Kimarekani waweze kuwachukua wana Diaspora kutoka USA na kwenda nao Tanzania kuwashirikisha kikazi.

        Aidha, mkutano huu uliwashirikisha Afisa Mkama, Suleiman Saleh na kampeni manager Mwanaidi “Mona”.   Kilicho shamiri kwenye mkutano huu ni washiriki wote kuwa na lengo linalo fanana; umoja, ushirikiano na amani.  Ndg. Mkama alisisitizia kuwa ni muhimu watu watoe michango ili waiwezeshe jumuia. Huku Ndg. Suleiman alisitia ushirikiano na umoja.
       
      Mwisho wa mkutano Ndg. Liberatus alimshukuru muheshimiwa balozi kwa kutumia muda wake wa thamani kuongea naye na kutoa shukrani za dhati kwa washiriki, Mh. Mkama na Suleiman.  Pia Ngd Liberatus aliwaomba kura washiriki wa mkutano huu; kwa bahati mbaya kura ilikuwa ni siri ya kila mmoja wao.  Zaidi, Liberatus alimshukuru Mh. Suleiman Saleh kwa niaba ya timu ya mpira kwa kushirikiana na wan DMV kwenye mechi za mpira wa miguu zilizopita.
Kwa habari, picha na sera za Liberatus BOFYA HAPA


Tunawatakia wana DMV uchaguzi wa HAKI NA AMANI na Ndg Liberatus anawaomba wana DMV mumpe FURSA

No comments: