Tumesikitishwa na upotoshaji wa Ndg.
Idd Sandaly alio utoa siku ya jana, July 4, 2014, juu ya timu ya Mgombea Urais
wa DMV Ndg. Liberatus Mwang’ombe “Libe”.
“Timu Libe for DMV Community President 2014” tunaomba Umma wa DMV na
duniani kote upuuzie upotoshaji wa Ndg. Sandaly kuwa tumekuwa tukifanya kampeni
za kutaka kumchafua. Tuhuma hizi ni za
uongo, uchochezi na zinalenga kubomoa jamii yetu ya DMV.
Tokea mgombea
Liberatus Mwangombe “Libe” achukue fomu za kugombea na jina lake kutangazwa na
tume ya uchaguzi; ametaja timu yake inayo undwa na watu wanne hadi hivi
sasa. Timu hiyo ya Ndg. Libe inaundwa
na;
Mwanaidi Love
“Mona”/kampeni meneja
Omby Nyongore/
Kampeni meneja msaidizi
Ebou Shatry aka
SwahilVilla/ Muandishi wa habari
Alawi Omari/
Strategist
“Timu Libe for DMV Community
President 2014” inapenda kuutaarifu Umma kuwa isihukumiwe wala kushirikishwa au
kuhusishwa na habari yeyote itakayo tolewa na mtu yeyote asiopo kwenye majina
tajwa hapo juu. Kinyume na hapo, ni
kutaka kuendeleza kampeni za kuchafuana; sisi hatuta kuwa na muda wa
kujibishana. Pia, tunapenda kuutaarifu
Umma kuwa “Timu Libe for DMV Community 2014” hatuna uwezo wa ku “control”
kinacho andikwa na watu kwenye mitandao ya kijamii. Zaidi, tunaheshimu haki ya kuzungumza mawazo;
“FREEDOM OF SPEECH.”
Kwa sasa, kampeni
zetu zimejikita kwenye kutafuta mbinu za kuiwezesha jamii ya DMV kuungana;
kuelezea sera zetu na sio kutenganishana.
UNITED
WE STAND; DIVIDED WE FALL
“Timu
Libe for DMV Community President 2014”
Imetolewa
na Mwanaid Love “Mona”/ Kampeni manager
No comments:
Post a Comment