Thursday, July 17, 2014

OFFICIAL STATEMENT: “TEAM LIBE FOR DMV PRESIDENT 2014” JUU YA DARASA LA KISWAHILI




     Tumesoma maelezo mkokotenga yaliyo andikwa na Ndg. Idd Sandaly ambayo hayana mashiko na kukosa mantiki kwa watu wenye weledi.  Maelezo hayo lukuki yaliyo kosa staha na nguvu ya hoja yanamshambulia mgombea wetu Ndg. Liberatus Mwangombe  kuhusu maoni yake juu ya darasa la Kiswahili.  Labda tuweke wazi kuwa; Ndg. Mwan’gombe habezi wala hapingi juhudi na uwezo ulio wekwa kuanzisha darasa la Kiswahili, la hasha! Liberatus anatilia shaka uwezo wa plani endelevu za kulidumisha darasa la Kiswahili. 

Ukweli usio pingika ni kuwa; darasa la Kiswahili lilisimama bila kutarajiwa na watoto wamekosa elimu ya Kiswahili kwa zaidi ya miezi sita.  Watoto hawa na wazazi wao hawajui tarehe ambayo darasa litarudi wala darasa litakuwa kwenye eneo gani.   Hili linathibitika kwenye maelezo ya Ndg. Idd Sandaly ambapo katika insha yake ya maneno zaidi ya 580; hakuna hata sehemu moja aliyo ainisha tarehe na sehemu ambayo darasa litarudi. Huu ni usanii wa waziwazi mchana kweupe. Ukweli mwingine unao umiza ni kuwa; ni zaidi ya miezi sita toka darasa lisimame na watoto wameshaanza kusahau yale walio fundishwa!

Maswali ya kimsingi ya kujiuliza ni kama yafuatayo:

Kufungwa kwa kanisa kulikuja kwa kushtukiza?
Je, tarehe ya darasa kurudi ipo wazi kwa watoto na wazazi?
Je, mitaala ya darasa la Kiswahili ilikuwa na “gap” ya miezi sita?
Je, uongozi ulikuwa na plan “B” baada ya mkataba wa kanisa kuisha?
Je, eneo la darasa ambapo litarudi (kwa madai ya Ndg. Idd Sandaly kwenye insha ya maneno ya zaidi 580) linajulikana kwa watoto na wazazi?

Jibu lolote la “Hapana” kwenye swali lolote hapo juu linadhihirisha kuwa liberaus Mwangombe yupo sahihi kuwa darasa la Kiswahili ni wazo zuri lakini lilikuwa na “poor planning” and “poor execution”

Team Libe for DMV President haitaongelea darasa la Kiswahili tena na inafunga huu mjadala kwa kusema, Darasa la Kiswahili ni wazo zuri, lakini lilikosa “SMART GOAL” (good planning) kwa sababu kuu moja; darasa la Kiswahili halipo tena! Wazazi na watoto hawajui litarudi lini na wapi.

Mwanaid Love “Mona” 
Team Libe for DMV Community President 2014 Campaign Manager

UNITED WE STAND; DIVIDED WE FALL



1 comment:

Anonymous said...

NAOMBA NIMJIBU ASHA NYANGANYI KAMA IFUATAVYO:

NIMEONA SHUTUMA NYINGI UNALENGWA WEWE KISTARABU ULUPASWA KUJIUZURU KWENYE TUME KAMA KWELI HUNA CHOCHOTE UNACHOPATA WHY HAUJIUZURU?

Mbili
KUSEMA KUWA WEWE UMEZALIWA NA
KUKUWA KWENYE PUBLIC HOME SIO KWELI LABDA UNAMDANGANYA HUYO IDD ASIYEKYJUWA
WEWE UMEISHI NYUMBA ZA SEREKALI RESIDENCE KAMA AMBAVYO WATANZANIA WENGINE WAMEKAA KWENYE NYUMBA ZA SEREKALI HIZO SIO PUBLIC HOME KAMA.UNAVYODAI UMEISHI NA KUZALIWA.MAY BE PUBLIC HOME NI HII YA UBALOZI KWA
MAWAZO YAKO NA HATA KAMA NI HIVYO UMEKAA ONLY 5 YEARS HUKUZALIWA HAPO AU KUKUWA HAPO KWA LEO NITAISHIA HAPA.TOA MASSAGE HII SIJAMTUKANA MTU NIMESEMA UKWELI BAADA YA KUONA ANAPOTOSHA JAMII NA UKWELI