Wednesday, June 18, 2014

Tuacheni "Mambo ya Matabaka" ili tuchaguwe Kiongozi anaekubalika DMV


Na Ebou Shatry

Sikiliza maneno ya Mgombea Urais DMV Liberatus Mwang'ombe wakati alipokuwa katika mjadala juu ya DMV. Kwamjadala mzima bofya  Hapa



Leo hii napenda kukumbusha tu kuhusu swali la ''ITIKADI'' yani ''UTABAKA'' Mhe Iddi Sandaly na timu kampeni yake swala la ''UCHADEMA'' lina wakereketa sana na kushika hatamu katika kampeni zao kumshambulia Mpizani mweza Liberatus Mwang'ombe "Libe" kwa mambo binafsi, hili halipendezi kabisa katika JUMUIYA yetu. Kumbuka, tulipigana kwa nguvu zote Media kuliondoa hilo akiwemo Liberatus Mwang'ombe  aliepanga mkakati mzima  kwa kushirikiana na media zetu kwa Mjadala wa Jumuiya zote za hapa DMV ili kukutana na kusuluhisha hilo katika mjadala uliofanyika siku ya jumamosi March 23, 2013 hapa Maryland.

Watanzania tunaoishi hapa DMV kama unakumbuka mwaka jana swali la utabakatulilipinga vikali katika kampeni za uchaguzi wa wa mwaka juzi 2012 mwazoni mwa mwezi April, Rais wa Jumuiya ya waTanzania Mhe. Idi Sandaly  ulishambuliwa sana katika swali la kuwa upande wa KIONGOZI wa Kiislamu na kuwatetea Jumuiya ya waIslam Tamco ya hapa DMV kitu ambacho naamini binafsikilikuwa ni ukiritimba tu wakuwania madaraka na kukufanya ushindwe katika kinyang'angiro cha uongozi uliokuwa unawania dhidi ya mpizani wako, nadhani mnakumbuka sana suala hilo ambalo nimeamua tumeamua kulifanyika kazi tukiwa kma watuza kumbukumbu zote za uchaguzi uliopita.

Pia suala la utabaka tulilifanyia kazi watu wa media kuliondoa hapa DMV, maana utabaka ulishika hatamu na likaleta mkawanyiko na ugovi mkubwa kwa upande wawanawake na wanaume waishio hapa DMV hadi wengine tukaambulia matusi katika media zetu, hatukuishia hapo tukaamua, kuwaita viongozi wa jumuiya zote za DMV ili kupatanisha migongano iliyotukabili wana jumuiya tunaoishi ha DMV kwa mambo hayo mnayoyafanya katika kampeni zetu kwa manufaa ya kumuondoa ama kumkandamiza LIBE, wakati Iddi alipokuwa madarakani juu ya uongozi wake alishindwa kulifanyia kazi ambae yeye ni kama Rais wa Jumuiya anastahili kutetea pande zote, bila ya mgawanyiko wa kitabaka kwa kuwakusanya watu pamoja kama walivyo hivi sasa baada ya kukutana viongozi hao kwa ushirikiano wa media zote za DMV.

Pia napenda kuwakumbusha Jumuiya ya watanzania DMV Katika mjadala huo wa Liberatus Mwang'ombe ndio aliesisitiza sana na kutaka viongozi wa jumuiya zote kupigania kuondoa mkawanyiko  uliokuwepo katika Jumuiya za waTanzania  baada ya ujio wa matawi ya vyama vya siasa kwa maana.

Katika mjadala huo Mhe Rais Iddi Sandaly ulikuwepo na akachangia maneno ya hikma na busara, mgombea wa urais 2014 Mhe Liberatus Mwang'ombe ambaye ni mmoja wa liosisitiza mjala huo alikuwepo kupitia uongozi wa CHADEMA, Bwn. RAYMOND ABRAHAM Makamu Rais. Jumuiya ya waTanzania DMV alikuwepo, Bwn. GEORGE SEBO kupitia Mwenyekiti Mpya wa (Tawi) CCM DMV, Bwn. nae piaYACOB KINYEMI Katibu wa Tawi CCM. DMV wakti huo alikuwepo, Bwn. Bwn. KESSY JANABI Rais Mstaafu wa Jumuiya DMV kwa miaka ya nyuma alikuwepo, Bwn. YUSUPH M. YUSUPH Mwenyekiti wa Jumiya ya kiIslamu, TAMCO, pamoja na Mch FERDNAND SHIDEKO wawa kanisa la (The way of the cross) nae pia alikuwepo, kuuondoa huu ukiritimba wa MADABAKA, jamani tusirudi kule tulipotoka tulifanya kazi ngumu kuondoa haya haya, JUMUIYA haina itikati ya aina yoyote bali wanajumuiya ndio wenye itikadi zao kwa hiyo tuheshimu itikadi ya mtu kabla hajafika katika jumuiya.


Mhe Rais, tunashukuru tulikuwa pamoja katika mazungumzo yalioelimisha wengi kwenye busara za kila kiongozi aliepata mualiko na fursa ya kuongea katika mjadala huo,  kwa hiyo tujaribu kusonga mbele kwa kuleta maendeleo huku tukiwa kila Mtanzania anaheshimu tabaka la mwezake.

Tujaribuni sana tusiwe wenye kurudi nyuma hayo mambo yashapitwa na wakati Liberatus Mwang'ombe (Libe)  ni mtu mwengine sasa tusitake kukumbusha kilio matangani, Liberatus Mwang'ombe sasa yupo kwaajili ya kuendeleza maendeleo ya Jumuiya ya DMVpale alopokosea kiongozi aliekuwa madarakani kwa miaka miwili bila ya maendeleo yakufaidika kwa wanajumuiya, tukiwa kama binaadamu hakuna asiekosea ama kuwa na sifa mbaya katika maisha yetu kutokana na binaadamu anajifunza kutokana na makosa.

Ombi langu kwenu ni  kuacha kabisa tendo la kuchafua Liberatus Mwang'ombe ambae anayetetea jahazi la jumuiya yetu kwenye maswala ya UTABAKA, Ukiwa Mkristo mwenye madhehebu tafauti hali kadhalika ukiwa Muislam tunapokuwa katika jumuiya yenye mchanganyiko wa watu tofauti tujaribuni kuondoa tofauti zetu.



No comments: