Wednesday, June 18, 2014

JE, NI NINI MGOMBEA URAIS DMV LIBERATUS MWANG'OMBE "LIBE" AMEIFANYIA DMV?

Na Liberatus Mwang'ombe

Audio clip hii hapa chini ni Mh. Idd Sandaly akikili mchango wangu kwenye michezo DMV kipindi cha kampeni za urais 2012. Mimi, Liberatus "Libe" nilikuwa namfanyia kampeni pia. Zaid, Mh. Sandaly anaahidi kuisadia timu ya mpira kifedha ili aiwezeshe timu kushiriki mashindano ya Diaspora World Cup.  FACT; baada ya Mh. Idd Sandaly kuchaguliwa jumuia iliipa kisogo timu ya mpira. Kwa maana, jumuia haija wahi kutoa hata sumni kwaajili ya timu. Ahadi hii haijatimilizwa hadi leo na imeendelea kuwa HEWA.


Nimeulizwa swali Viber na Aunt Ashura, hili swali limekuwa likijirudia rudia na limekuwa gumzo kwenye comments za Vijimambo; swali lenyewe ni hili
"Libe, unataka urais DMV, ukiacha uliyo yafanya nyumbani, Tanzania, ni nini umefanya DMV ?"
Pia, kuna mtu amenipigia simu na kuniuliza swali kuwa huwa ninachangia misiba lakini sihudhurii.

Majibu yangu ni kama ifuatavyo;
Kwanza kabisa, nilikuwa nimepanga kuto ongelea maswala ya misiba kwani sitaki kuchoma hisia za watu walio athirika na kupata msongo wa mawazo kwa kuondokewa na wapendwa wao wa moja kwa moja.  Wiki iliyopita dada Asha Nyang’anyi alituasa tusiongelee misiba kwani ni kutonesha vidonda na machungu ya ndugu wa marehemu.  Naheshimu mawazo ya Dada Asha, lakini kama hili swala la misiba litaendelea kuleta sintofahamu; nitalijibu.

Sasa naenda kwenye hoja ya msingi: Nini nimeifanyia DMV? 

-Mosi, nimesha mtoa mTanzania jela kwa kumuweka bond ( jina linahifadhiea na litatolewa ikibidi)
-Pili, nimekuwa nikishirikiana na DJ Lu kuipeleka team ya DMV (Soccer) nje ya State kifedha na uchezaji
-Tatu, mwaka 2013; nimeiwezesha team ya TANZANIA kushiriki league kwa kuchangia zaidi ya $1,000.00 (Approximately $1,500.00) kutoka mfukoni mwangu
Hapa ni baada ya kuiwakilisha DMV North Carolina na kurudi na kombe. Tulilikabidhi kombe kwa Balozi Mwanaid Maajar na yeye alitukabidhi rasmi Mirage Hall

-Nne, nime isaidia team ya mpira Tanzania DMV mwaka huu kwa kutoa $500.00 ili kushiriki Diaspora World Cup
-Nne, Nimewachangia waTanzania walio wekwa jela immigration (Majina kapuni, yatatolewa itakapo bidi)
-Tano, kwenye jumuia part 2012 ya mwisho wa mwaka nilishiriki kufanya usafi baada ya kumalizika party nikiwa mimi, Didi Vava, Evans na wengine. Viongozi wengine walitoweka
-Sita, kwenye party ya mwaka huo huo 2012 nilikabidhiwa idara ya ulinzi pale ndani
Houston TX baada ya kuifunga Serengeti
Bosy na kuchukua kikombe nikiiwakilisha DMV
-Saba, nimewawezesha waTanzani watatu kupata I-20 ( Hawa wapo out of the state)
-Nane, nimewapeleka baadhi ya waTanzania kwenye test MVA na gari yangu; bure (names are enclosed). Yatatolewa ikibidi
-Saba, Nimeweza ku-empower baadhi ya waTanzania kwenda college; wengine wapo college sasa na mmoja amegraduate
-Nane, nimeweza ku co-sign watu ili wapate makazi (majina kapuni)
-Tisa, nilisimamia mashindano ya Vijimambo soccer 2012 ambapo DC Nyarugusu ilikuwa bingwa
-Kumi, nimekuwa nikijitolea kufundisha mpira wa miguu kwa watoto chini ya miaka 19, 14 na 7 kwa zaidi ya miaka saba. ( Ukihitajika ushahidi nitaleta barua ya wazi kutoka kwa kocha wangu wa shule)

Siku tulipo chukua kombe North Carolina baada ya kuifunga Sierra Leone kwenye final 

Mwisho, naomba na nawahasa watu wa upande wa pili tufanye kampeni kwa hoja na sio kushambuliana binafsi na kuzushiana mabo ya uongo. Uchaguzi huu ni fursa kwa wana DMV kuwa na uchaguzi wa kihistoria na wenye mvutano mkubwa wa hoja. Lets practice real democracy 2014!

Libe akiendelea kuiwakirisha DMV  na kuitangaza Tanzania dhidi ya Liberia

No comments: