Tuesday, June 24, 2014

JUA IMANI YA MSINGI YA MGOMBEA WAKO WA URAIS WA DMV, USA, LIBERATUS MWANG'OMBE “LIBE”

Na Liberatus Mwangombe “Libe”
            Nikirudisha kidogo nilicho nacho kwenye jamii yangu
Tokea maisha yangu ya utotoni nakumbuka kuwa na hamu, uchungu na kutambua umuhimu wa kubadilisha maisha ya watu wanao nizunguka katika hali bora endelevu.  Imani yangu ya kimsingi na niliyo kuzwa nayo, ni juu ya uwezo wa binadamu mmoja kumsaidia mwenzake mwenye hitaji, inanisukuma na kuchochea kujitolea nafsi yangu kuwatumikia binadamu wenzangu. 

        Imani hii ya utumishi ilijengwa kwangu na malezi ya mama na baba yangu mzazi.  Wazazi wangu wamenilea kwenye mazingira ya kiubinadamu; yaani, ninapo muona mwenzangu kadondoka chini, nisimcheke, bali nimshike mkono na kumsaidia kunyanyuka.
         Imani hii ya kutaka kusaidia na kubadilisha maisha ya watu ndani ya moyo wangu iliongezeka kwa
kasi pale mwalimu wangu wa somo la “Public Health” (MPH) alipo tushauri tuangalie sinema inayo itwa “I AM”.  Hii sinema ilibadilisha mtazamo wangu wa maisha juu ya uwepo na madhumuni ya binadamu kwenye ulimwengu huu.  Mazingira ya sinema hii ni kumuwekea hadhira maswali na atafute utatuzi wake.  Mfano wa maswali ni, “What’s wrong with this world”?.  Zaidi, sinema hii inamtaka hadhira kutafuta jawabu la swali hili na kulitatua. 
Nikiwa na dada yangu wa kwanza tukirudisha kidogo tulicho nacho kwenye jamii tuliyotoka

Baada ya kuangalia hii sinema; nilianza kujiuliza maswali kama “what’s wrong with the world” (Tatizo la dunia hii ni nini) “What’s human nature? (Nini asili ya binadamu)” “Are we born to cooperate with each
other or compete with one another” ( Tumezaliwa ili tusaidiane au tushindane), “Is basic health care a human right or a commodity?” (Huduma ya afya ni haki ya binadamu au ni biashara), “Is death your only option because you can not afford health care?” (Kifo ni njia pekee kama huwezi kulipia matibabu).  Baada ya kuangalia na kutafakari maswali haya kinagaubaga; nilijiona bado nina deni kubwa na jamii yangu ya KiTanzania.  Kutokea hapo, ile imani yangu ya kimsingi niliyo kua nayo toka nikiwa mdogo ilichochewa na nimeendelea kuchukua hatua kuwasaidia watu wanao nizunguka.
Baba yangu na familia yangu ilikuwepo kwenye kurudisha kidogo tulicho jaliwa kwenye jamii yetu
         
     Mwaka 2008 nilitembelea nyumbani, Tanzania, ambapo nilishuhudia watoto wadogo wakitanzania kati ya miaka 7 hadi 14 wakiishi maisha ya kubahatisha na kusikitisha ya mtaani.  Zaidi nilishuhudia baadhi ya hawa watoto waki vuta sigara.  Tatizo hili ni la kutisha kwa sababu kuu moja; kuto kuwa na habari sahihi juu ya matumizi ya tumbaku.  Pia nimeshuhudia watoto wakizaliwa na UKIMWI (HIV/AIDS) kwa sababu kuu moja tu; mama ameshindwa kulipia huduma bora ya uzazi (mother didn’t have access to quality prenatal care). 
Zaidi, vijana ambao maumbile yao yanawawezesha kujamiina hawana elimu juu ya gonjwa hili hatari la UKIMWI.  Pia, Elimu nyepesi kama kuosha mikono ambayo watoto wa hapa tulipo, USA, wanafundishwa majumbani na mashuleni; jamii yetu imeikosa! Nasikitika kumtaarifu msomaji kuwa; jamii yetu ya kiTanzania inateketea kwa magonjwa ambayo yanaweza kutibika ( Managable diseases)
         Baada ya kurudi USA mwaka ule (2008) na kuendelea kupiga “box” huku nikienda shule na kujisomesha kutoka mfukoni; nimekuwa nikitafakari matatizo niliyo yaona nyumbani kwa kina.  Tafakuri hili jadidi limekuwa likichochewa na ile imani yangu ya kimsingi ya kuwasaidia watu wanao nizunguka.  Pia, kwenye imani hii ambayo ipo ndani ya moyo wangu, imekandamizwa na ukweli wa asili kuwa binadamu tuliumbwa tushirikiane na sio tushindane na tutengane.  Nipo tayari na nimejitolea maisha yangu kuwasaidia binadamu wenzangu kwa chochote nilicho nacho na kufanya maisha yao tofauti katika hali bora endelevu.
         Kwa historia hii fupi ya “LIBERATUS MWANG’OMBE “LIBE” NI NANI; napenda kutumia walaka huu kujitambulisha kwa waTanzania wote wa DMV kuwa nina gombea nafasi ya Urais wa jumuhiya ya Tanzania hapa DMV, USA.  Ninaomba ushirikiano wenu na kura zenu ifikapo siku ya uchaguzi July 20, 2014.  Nina ahidi katu sito waangusha.  Nitafanya kazi bila kuchoka, usiku na mchana kuhakikisha ile imani yangu ya kimsingi ya; “binadamu mmoja kumsaidia mwingine” ninaendelea kuitekeleza katika kipimo kipana.  Kikubwa kinacho tokana na hii imani yangu ni kuwa “SIPO HAPA KUSHINDANA BALI KUSHIRIKIANA NA KUDUMISHA UBINADAMU”
Nikiendelea kufurahia wakati na watoto nilipo watembelea na kuwahimiza kusoma kwa vidii

Naitwa Liberatus Mwang’ombe “Libe” kwa unyenyekevu wa dhati naomba tushirikiane na unipigie kura
Asante sana kwa kusoma historia yangu fupi ya imani yangu ya kimsingi
Libe for The DMV Community President 2014











Naitwa Liberatus Mwang’ombe “Libe” kwa unyenyekevu wa dhati naomba tushirikiane na unipigie kura

Asante sana kwa kusoma historia yangu fupi ya imani yangu ya kimsingi
Libe for The DMV Community President 2014



No comments: