Na Liberatus Mwang'ombe
Liberatus believes
"CHARITY STARTS AT HOME"
Katika
muendelezo wa kusaidia nyumbani kama imani yangu ya kimsingi; ninaamini kuwa, “binadamu
tulizaliwa tushirikiane na tusaidiane kutatua matatizo na sio kutengana wala
kushindana.” Kwenye safari yangu ya Tanzania 2011 na 2013 nilipata fursa ya
kutembelea hospital za Muhimbili na Aga Khani zilizopo Dar Es Salaam, na
hospital ya Muhimbira iliyopo kijijini kwetu Chimala, Mbeya. Kwenye hospital ya Muhimbili na Aga Khan
niliongozana na Dr. Leslie Kingslaw (A Pulmonologist from Wshington Hospital and
Providence Hospital) na Ms. Kingslow (Nurse practitioner).
Muhimbili na
Aga Khan, year 2011
Katika
safari hii Dr. Kingslaw alitoa somo juu ya ugonjwa wa Chronic Obstractive Pulmonary
Disease (COPD) unao sababishwa na uvutaji wa sigara kwa asilimia kati ya
80-90%. Ugonjwa huu husababishwa pia na
mambo mengine, kama vile, genes, historia ya familia, kazi unayofanya na mazingira;
lakini husababishwa na utumiaji tumbaku (sigara) kwa asilimia kati ya 80-90%.
Libe akiwa na Mr. & Ms. Kingslow na daktari wa Aga Khan baada ya lecture
Baada
ya kutoa somo juu ya gonjwa hili, COPD, tuliweza kutoa vipimo vya oxygen kama
msaada. Vipimo hivyo vinaitwa “pulse
oximetry”. Vile vile nilipata
kubadirishana mawazo na madaktari wa Muhimbili na Aga Khan. Katika mabadirishano ya mawazo; nilishtushwa
na ukweli kuwa kuna watu hupoteza maisha kwa sababu tu, hawawezi kulipia mtungi
wa oxygen! Baada ya mazungumzo hayo; nilirudi USA na kuendelea kupiga “box”
huku nikitafakari jinsi ya kutatua matatizo haya. Bado tafakuri hili linaendelea na naomba
ushirikiano wa waTanzania wote waliopo USA kufanya jambo lolote kwaajili ya
nyumbani.
Safari ya hospital ya
Muhimbira Chimala Mbeya, year 2013
Juu na chini Liberatus anarudisha kidogo alicho nacho kwenye hospital ya kijijini kwao
Hii
ni kati ya hospital masikini nilizo tembelea.
Niliona mengi ambayo yanatakiwa kuwezeshwa. Hospital ya Muhimbila hutoa huduma kwa watu
zaidi ya 20,000 kwa mwaka! Hospitali hii inaupungufu wa vifaa mbalimbali vya
kutendea kazi; kama vile, vitanda, sindano, dawa za maleria, vipimo vya X-ray,
oxygen tanks n. k. Hii ni hospital
niliyo kuwa natibiwa maleria kipindi nikiwa mdogo. Sikusita kupita na kutoa kidogo nilicho
jaliwa. Nilipo enda nyumbani mwaka 2011
waliniambia kuwa wanaupungufu wa vifa vya kutendea kazi, kama vile kipimo cha “Blood Presssure”. Mwaka 2013 nilipo kwenda niliwapelekea kipimo
hicho cha mapigo ya damu na chenye uwezo wa kupima “heart rate”. Daktatri na wauguzi (nurses) walifurahi sana.
Asante sana kwa kusoma
makala yangu fupi ya kutembelea hospitali nyumbani
Tanzania
Naitwa Liberatus Mwang’ombe “Libe” kwa
unyenyekevu wa dhati naomba tushirikiane na unipigie kura
Libe for The DMV
Community President 2014
No comments:
Post a Comment