Na Ebou Shatry
Mkaazi mkongwe katika Jiji la Washington D.C. Bwana Doto Mallongo siku ya Jumatatu June 23 amefanikisha kulipa ada yake ya uwanachama hai baada ya kukutana na Jabiri Jongo, ambae ni Mjumbe wa tume ya uchaguzi wa Jumuiya ya waTanzania DMV ili kujianda kwa ajili ya maandalizi ya kinyang'ang'anyiro cha uchaguzi ujao utakaofanyika Julai 21, 2014

Mkazi wa mkongwe wa DMV bwana Doto Mallongo akimkabizi pesa taslim Bwna Jabiri Jongo ambae ni Mjumbe wa tume ya uchaguzi wa Jumuiya ya waTanzania DMV na kuwa Mwanachama hai wa jumuiya.
Bwana
Doto kwa uthipitisho wa kufuata sheria hizo za katiba na kuwa mwanachama hai,
alisisitiza sana watu kulipa ada ya uwanachama hai ili wapate fursa ya uchaguzi
wakupiga kura na kumchagua kiongozi wanaemtaka, Doto Mallongo aliyasema hayo
akiwa mmoja wa wanachama wajumuiya jijini hapa anaetaka mabadiliko dhidi ya
uongozi uliopita, kwa utekelezeaji wa sheria za katiba ya Jumuiya ya waTanzania
DMV
Baada
ya kulipa ada yake ya kuwa mwanachama hai, aliwataka tume ya uchaguzi wa
Jumuiya ya waTanzania DMV kuwa makini sana na maamuzi binafsi ambayo yanafanywa
kwa ukiukwaji wa katiba bila ya kushurutisha pande nyingine, ambapo kwa hivi
sasa tayari maswali mengi yameanza kujitokeza dhidi ya ukiukwaji wa sharia
katika mchakato wa uchaguzi utakaufanyika mwishoni mwa mwenzi ujao.
No comments:
Post a Comment