Liberatus "Libe"/ mgombea nafasi ya Urais
Team Libe for DMV Community
President 2014 tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa kila mmoja aliye weza
kufika kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara jana Meadowbroak Park. Pia
tunapenda kuwashukuru wale walio kuwa na nia ya kuja lakini kwa sababu zilizo
nje ya uwezo wao wakashindwa kutimiza hadhma hiyo. Asanteni!
Pia, Team Libe for DMV Community
President 2014 tunapenda kuwashukuru wagombea wengine kwa kujitokeza na kuonyesha
ushirikiano chanya na kufurahia mazungumzo na wapiga kura; asante mama Salma
Manyoka/mgombea makamu wa Rais, asante Heriet Shangarai/ mgombea makamu wa Rais,
asante Solomon Cris/mgombea makamu wa katibu
Zaidi, shukrani zetu za dhati
zinaenda kwa Ndg. Hamza Mwamoyo/Mwenyekiti wa board, Mzee Safari/ Mkiti wa tume
ya uchaguzi na mke wake mama Safari, kaka yetu Jabil Jongo/ mjumbe tume ya
uchaguzi na mchungaji Malekela kwa kuonyesha mapenzi yasio na ukomo kwa jumuia
yetu ya DMV.
Mwisho, tunawashukuru wana DMV
wote kwa kuwa na ushirikiano thabiti na kusaidiana kwenye raha na shida. Kama
imani ya kimsingi ya “, Team Libe for DMV Community President 2014” inavyo sema
“binadamu tupo hapa ili tushirikiane na sio kushindana wala kutengana”
Team Libe for DMV Community
President 2014 wishes all Muslim Ramadan Karim.
Have a wonderful
weekend
Picha na Ebou Shatry/Swahilivillablog
No comments:
Post a Comment