Sunday, June 29, 2014

PICHA: ULIVYO KUWA MKUTANO WA MGOMBEA LIBERATUS MWANG'OMBE "LIBE"

 Mgombea wa Urais Ndg Liberatus Mwang'ombe "Libe"
 Mgombea wa makamu wa Rais Bi Salma Mushi
 Mgombea wa makamu wa katibu Ndg Solomon Cris
Mgombea wa makamu wa Rais Bi Heriet Shangarai
  Ndg Victor kushoto akiwa na Team Libe kampeni strategist Alawi Omari

     Ndg Alex Kasuwi akiwa na mwanawe kwenye kampeni
 Ndg dotto Mallongo akiuliza swali huku akiwa na mwanae
   Kutoka kushoto; Bi Salma Moshi, Mchungaji Malekela, Mzee Muganda na Hamza Mwamoyo
 Wgombea wa makamu wa Rais wakiwa kwenye picha ya pamoja
  Bi Quizella Mtagazwa akiuliza swali huku Mona akisikiliza kwa makini
 Mgombea wa Rais Liberatus "Libe" mwenye tai nyekundu na Ebou mzee wa SwahiliVilla
 Jacky akiwa na mama yake kwenye mkutano 
   Samweli Mwimanzi akiwa kwenye mitambo

  Wageni wa kila aina walikuwepo


 David Ndunguru alikuwepo
 Beybe Mgaza naye alikuwepo
 Mona akiuliza swali

 Samweli Mwimanzi akifuatilia mkutano kwa makini

                                                Team Libe kampeni strategist Alawi Omari

Picha: Ebou Shatry/ Swahilivilla Blog

Mkutano wa Sera za Liberatus Mwang'ombe June 28, 2013



Video: Ebou Shatry/ Swahilivilla blog

SHUKRANI: TEAM LIBE FOR DMV COMMUNITY PRESIDENT 2014

Liberatus "Libe"/ mgombea nafasi ya Urais
Team Libe for DMV Community President 2014 tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa kila mmoja aliye weza kufika kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara jana Meadowbroak Park. Pia tunapenda kuwashukuru wale walio kuwa na nia ya kuja lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao wakashindwa kutimiza hadhma hiyo.  Asanteni!

Pia, Team Libe for DMV Community President 2014 tunapenda kuwashukuru wagombea wengine kwa kujitokeza na kuonyesha ushirikiano chanya na kufurahia mazungumzo na wapiga kura; asante mama Salma Manyoka/mgombea makamu wa Rais, asante Heriet Shangarai/ mgombea makamu wa Rais, asante Solomon Cris/mgombea makamu wa katibu
 
Mama Salma/Mgombea makamu wa Rais
Zaidi, shukrani zetu za dhati zinaenda kwa Ndg. Hamza Mwamoyo/Mwenyekiti wa board, Mzee Safari/ Mkiti wa tume ya uchaguzi na mke wake mama Safari, kaka yetu Jabil  Jongo/ mjumbe tume ya uchaguzi na mchungaji Malekela kwa kuonyesha mapenzi yasio na ukomo kwa jumuia yetu ya DMV.
 
Heried Shangarai/Mgombea makamu wa Rais
Mwisho, tunawashukuru wana DMV wote kwa kuwa na ushirikiano thabiti na kusaidiana kwenye raha na shida. Kama imani ya kimsingi ya “, Team Libe for DMV Community President 2014” inavyo sema “binadamu tupo hapa ili tushirikiane na sio kushindana wala kutengana”


Solomon Cris/Mgombea makamu wa katibu

Team Libe for DMV Community President 2014 wishes all Muslim Ramadan Karim.


Have a wonderful weekend
Picha na Ebou Shatry/Swahilivillablog

Tuesday, June 24, 2014

URAIS DMV, USA: LIBERATUS MWANG'OMBE "LIBE" KUUNGURUMA JUMAMOSI JUNE 28, 2014





Jumamosi, June 28, 2014 kuanzia saa 10 alasiri (4pm) 
Meadowbrook Park 
 7901 Meadowbrook Lane Chevy Chase, MD 20815

Maswali: Alawi Omari/Campaign strategist 301 339 3765 
Liberatus mwangombe "Libe"/ President candidate 240 423 3331 
Video: Ebou Shatry Swahilivilla 301 728 3977

Doto Mallongo mwanachama hai wa Jumuiya ya waTanzania DMV

Na Ebou Shatry

Mkaazi mkongwe katika Jiji la Washington D.C. Bwana Doto Mallongo siku ya Jumatatu June 23 amefanikisha  kulipa ada yake ya uwanachama hai baada ya kukutana na Jabiri Jongo, ambae ni Mjumbe wa tume ya uchaguzi wa Jumuiya ya waTanzania DMV ili kujianda kwa ajili ya maandalizi ya kinyang'ang'anyiro cha uchaguzi ujao utakaofanyika Julai 21, 2014

Mkazi wa  mkongwe wa DMV bwana Doto Mallongo akimkabizi pesa taslim Bwna Jabiri Jongo ambae ni Mjumbe wa tume ya uchaguzi wa Jumuiya ya waTanzania DMV na kuwa Mwanachama hai wa jumuiya.

Katika harakati hizo za maandalizi ya  uchaguzi uliopangwa kufanyika Julai 20,  mwaka huu, kwa mujibu wa sheria ya katiba ya Jumuiya ya waTanzania DMV, waTanzania wote wanapaswa kuwa wanachama hai ili wajipatie fursa ya upigaji kura na kumchagua kiongozi wanaemtaka 

Bwana Doto kwa uthipitisho wa kufuata sheria hizo za katiba na kuwa mwanachama hai, alisisitiza sana watu kulipa ada ya uwanachama hai ili wapate fursa ya uchaguzi wakupiga kura na kumchagua kiongozi wanaemtaka, Doto Mallongo aliyasema hayo akiwa mmoja wa wanachama wajumuiya jijini hapa anaetaka mabadiliko dhidi ya uongozi uliopita, kwa utekelezeaji wa sheria za katiba ya Jumuiya ya waTanzania DMV

Baada ya kulipa ada yake ya kuwa mwanachama hai, aliwataka tume ya uchaguzi wa Jumuiya ya waTanzania DMV kuwa makini sana na maamuzi binafsi ambayo yanafanywa kwa ukiukwaji wa katiba bila ya kushurutisha pande nyingine, ambapo kwa hivi sasa tayari maswali mengi yameanza kujitokeza dhidi ya ukiukwaji wa sharia katika mchakato wa uchaguzi utakaufanyika mwishoni mwa mwenzi ujao.




URAIS DMV, USA: LIBERATUS MWANG'OMBE "LIBE" KUUNGURUMA JUMAMOSI JUNE 28, 2014



Jumamosi, June 28, 2014 kuanzia saa 10 alasiri (4pm)
Meadowbrook Park

7901 Meadowbrook Lane
Chevy Chase, MD 20815
Maswali: Alawi Omari/Campaign strategist 301 339 3765
Liberatus mwangombe "Libe"/ President candidate 240 423 3331
Video: Ebou Shatry Swahilivilla 301 728 3977

LIBERATUS "Libe" MWANG’OMBE, MPH, BSRC, RRT-NPS.
Intern:The Division of Health Interview Statistics (DHIS) at the National Center for Health Statistics (NCHS)/United States  Center for Disease Control and Prevention (CDC)


Ushirikiano na Umoja
  •  Uongozi huu utaimarisha ushirikiano  na ubalozi wetu pamoja na wizara ya mambo ya nje, ili kupendekeza “Diaspora policy” itakayowapatia wanaDispora nafasi za kazi, mikopo nchini Tanzania na kuwezesha uraia pacha.
  • Pia tutahakikisha waTanzania  wanapatiwa fursa ya kuongea na viongozi wa serikali wakiwa kwenye ziara hapa USA, ili kujadili mambo mbali mbali  yanayoendelea nchini.
  • Mapendekezo ya  kurekebishwa kwa katiba yatafanyika awali,  ili kulinda haki za wapiga kura DMV  (Kupiga kura iwe haki kwa kila mTanzania na sio "benefit", yaani sio pay-register and vote)
  • Uongozi huu utafanya maamuzi kwa kufuata katiba ili kuleta amani, umoja na mshikamano.
  • Uongozi huu utakuwa wa uwazi na ukweli. “UWAZI na UKWELI”  ni msingi wa Imani na kichocheo cha Uzalendo
  • Katika uongozi wetu kila Mtanzania atapewa heshima stahiki na haki ya kusikilizwa na kushirikishwa 
Baraza la Ushauri
  • Uongozi huu utatambua mchango wa viongozi waliopita, viongozi  wa dini  na  wazee na kuwajumuisha katika  baraza la ushauri.  

Lugha ya Kiswahili
  • Uongozi huu unatambua mchango mkubwa uliofanywa wa kuanzishwa kwa darasa la kiswahili na utafanya juhudi za kuendeleza juhudi hizo.
  •  Nia yetu ni kukuza kitengo hiki kwa kuwakaribisha watu wa mataifa mengine  kujifunza lungha yetu ya  Kiswahili   ambayo imekubalika rasmi kwenye Umoja wa Afrika
  • Uongozi huu utajihusisha na shule za sekondari pamoja na vyuo nchini  Marekani vinavyofundisha lugha ya Kiswahili kwa nia ya kuwapatia wanajuiya ajira ya walimu na ukalimani wa lugha ya kiswahili.
Jumuiya na Wajasiriamali
  • Uongozi wetu utatumia  Association of Tanzania Community (ATC) kuwadhamini wajasiriamali   kupata mikopo midogo na mikubwa ya  kufungua biashara zao.
  • Ili kuwawezesha wajasiriamali, tutaweka taratibu za kuwapatia  mafunzo  na kufwatilia maendeleo ya biashara zao. 
Elimu 
  •    Uongozi utachukuwa jukumu la kuhakikisha kuwa, Watanzania wanapata taarifa sahihi za udhamini wa elimu  wa vyuo mbalimbali na fursa nyingine kama “Young African Leaders Initiatives” (YALI), juhudi za Rais Baraka Obama kusaidia viongozi wa kesho barani Africa. Uongozi utatoa habari ya bahati nasibu “Diversity Visa Lottery” kwa Watanzania wanotafuta fursa ya kusoma na kujiendeleza hapa Marekani.

Jumuia na vyanzo vya mapato
  •  Mapato ya jumuiya yatatokana na ‘fund rising events’ tukishirikisha mataifa mbali mbali pamoja na miradi midogo katika shuhuli hizo.
  •   Kwa kutumia hadhi ya 503 (c) tutatafuta misaada kutoka mashirika makubwa na hospitali  ili kupata  vifaa kwa ajili ya hospital za nyumbani.

Jumuia na Afya

  •   Tutaanzisha “Nursing Association” kwenye jumuia  ambayo itakuwa ikitoa mafunzo.  Pia tutatafuta namna ya kupata unafuu wa Health Insurance kama kikundi ili kupunguza gharama