Sunday, October 4, 2015

MWANA DIASPORA KUTOKA MAREKANI AENDELEA KUZOA UMAARUFU MBIO ZA UBUNGE

Ni Liberatus Mwang'ombe "Libe" ameendelea kuwa mwiba kwa wagombea wengine kwa kukusanya makundi ya aina mbalimbali, watoto, wazee, vijana na kinamama. Mh. Mwang'ombe amekua akitoa hotuba kwa uhodari wa hali ya juu na kuwafanya watu wa Mbarali kuwa na matumaini na kujisikia wapo wamoja.

Moja ya kipengele chake kweye hotuba kinacho wavutia watu ni pale anapo sema "hatuunganishwi kwa itikadi zetu, vyama vyetu, jinsia zetu, dini zetu wala makabila yetu; bali tunaongunishwa kwa changamoto zinazo tuzunguka, changamoto za maji, afya, ardhi, TANAPA, miundombinu, elimu na afya. Hizi ndio kero zinazo tufanya tuwe wa moja na tukapige kura kumchagua mtu sahihi wa kuzisimamia, mtu huyo sio mwingine bali ni Liberatus Laurent Mwang'ombe".


Libe anawaomba wana diaspora na waTanzania wote kumuunga mkono kwa kumchangia fedha ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mtunga sheria Tanzania. Msaada wa fedha anaomba utumwe kupitia;

M-PESA- WAVE App number +255 752 494 409

Au, wasiliana na: 
Rehema Sarmet 301 367 9711
Lukresia  240 593 5973
Jabil  240 604 0574



 Juu na chini: Mh. Mwang'ombe akibadirishana mawazo na watoto wa darasa la sita ambao walimfuata kila anako kwenda baada ya mkutano


 Mh. Mwang'ombe hupita kila kona, kwenye vijiwe, vilabu vya pombe, madukani kabla na baada ya mikutano yake kusalimiana na wadau
Juu na chini: Mh. Mwang'ombe akiendelea na mkutano hapo jana

Juu na chini: Watoto, watoto wanapenda Libe



No comments: