Friday, October 16, 2015

BREAKING NEWS: MAMA REGINA LOWASSA USO KWA USO NA MWANA DIASPORA, LIBERATUS MWANG'OMBE

Mama Regina Lowassa leo alikuwa Chimala, Mbarali akimnadi mgombea ubunge jimbo la Mbarali, Liberatus Mwang'ombe "Libe". Akiongea na wana Mbarali mama Lowassa amesema mwang'ombe ni kijana mweledi, msomi, na mwenye maono na Mbarali; hivyo basi amewaomba wana Mbarali wasimpoteze Mh. Mwang'ombe. 

Mama Lowassa alishangazwa na umati uliojitokeza baada ya taarifa ya masaa matutu kuwa atasimama Chimala. Mh. Mwang'ombe akitoa shukrani zake kwa mama Lowassa kufika Mbarali alisema "Mbarali ina wapiga kura 143189 na watu wa Mbarali wameonyesha kila dalili ya kutaka mabadiliko". Mwang'ombe aliwaomba watu wa Mbarali wampeleke Dodoma akihutubia na kuwasisitiza wajitokeze kwa wingi Jumapili, tarehe 18/10/2015 saa 3 asubuhi ambapo Mh. Lowassa atakuwa anaunguruma naye. 

Mama Lowassa na Mh. Mwang'ombe katika ubora wao

 Mh. Mwang'ombe anakubalika Mbarali, hapa umati ukiwa umezingira gari lake lisiondoke
 Watu wa ,barali wanataka mabadiliko

Libe anawaomba wana diaspora na waTanzania wote kumuunga mkono kwa kumchangia fedha ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mtunga sheria Tanzania. Msaada wa fedha anaomba utumwe kupitia;

M-PESA- WAVE App number +255 752 494 409

Au, wasiliana na: 
Rehema Sarmet 301 367 9711
Lukresia  240 593 5973
Jabil  240 604 0574 

No comments: