Tuesday, October 13, 2015

MBIO ZA UBUNGE: LIBERATUS MWANG'OMBE AENDELEA KUWA KIMEO KWA WAGOMBEA WENZAKE

Nyota ya mwana-diaspora kutoka Marekani inaonekana kung'aa kwenye mbio za ubunge mwaka huu. Ni Liberatus Mwang'ombe "Libe" ambaye amekuwa akijizolea umaarufu kila uchao. Mh. Mwang'ombe amekuwa akivunja rekodi kila siku kwa kuwa na mvuto kwenye mikutano yake kuliko mgombea yoyote aliye wahi kutokea kwenye historia ya jimbo la Mbarali.

Mh. Mwang'ombe anaye onekana kuwavutia watu wa rika mbalimbali amekuwa changamoto kwa wagombea wengine ambao kuna baadhi ya maeneo wameshindwa kufanya mikutano kwa kukosa watu na kuzomewa pale wanapo msema Mwang'ombe. Zaidi, mgombea wa ACT, Modestus Kilufi,  alikutana na dhahama baada ya kujaribu kumsema vibaya Mh. Mwang'ombe kwenye kijiji cha Chimala ambapo ndipo alipo zaliwa Mwang'ombe.  Mh. Kilufi alipo jaribu kuanza siasa za kumponda Mwang'ombe zilisikika sauti za watu wakipiga kelele na kusema kama unamsema huyo shuka jukwaani na ondoka. 

Baada ya kuona hasomeki,  Mh.Kilufi akabadilisha maneno na kuwaambia watu wa Chimala kuwa "kama hamta nipa kura mimi, msimpe Haroon (mgombea wa CCM), bora mpeni kijana Mwang'ombe". Baaada ya maneno hayo umati wa watu ulilipuka kwa shangwe




Libe anawaomba wana diaspora na waTanzania wote kumuunga mkono kwa kumchangia fedha ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mtunga sheria Tanzania. Msaada wa fedha anaomba utumwe kupitia;

M-PESA- WAVE App number +255 752 494 409

Au, wasiliana na: 
Rehema Sarmet 301 367 9711
Lukresia  240 593 5973
Jabil  240 604 0574 





No comments: