Thursday, October 8, 2015

BREAKING NEWS: KIJANA KUTOKA MAREKANI AENDELEA KUWA GUMZO MBIO ZA UBUNGE

Ni Liberatus Mwang"ombe "Libe" ambaye anaonekana kuzoa umaarufu kila uchao kwa weledi wake wa kutoa hotuba zenye kuwaleta watu pamoja na kuwaita vijana katika siasa. Mh. Mwang'ombe amekuwa gumzo jimboni Mbarali kiasi kwamba amekuwa akisimamishwa na watu mbalimbali mitaani hadi wanafunzi. Leo akifanya mkutano wa kampeni Rujewa ameweza kukusanya watu wengi na kusindikizwa na msafara baada ya mkutano hadi ofisi za CHADEMA wilaya. 






Kwenye hotuba yake Mh. Mwang'ombe amesisitizia umoja, ushirikiano na maslai ya Mbarali bila kujari mlengo wa chama wala itikadi. Ameweza kutoa historia ya Mbarali kuanzia kipindi cha mbunge wa kwanza kwenye jimbo hilo Mh. Kanali Mjengwa na kueleza namna alivyo isaidia Mbarali. Uwezo wa Mh. Mwang'ombe kuelezea historia ya Mbarali kumewakuna wengi na wametoka kwa kauli moja kuwa "2015" ni mwaka wa Mwang'ombe

Libe anawaomba wana diaspora na waTanzania wote kumuunga mkono kwa kumchangia fedha ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mtunga sheria Tanzania. Msaada wa fedha anaomba utumwe kupitia;

M-PESA- WAVE App number +255 752 494 409

Au, wasiliana na: 
Rehema Sarmet 301 367 9711
Lukresia  240 593 5973
Jabil  240 604 0574



No comments: