Liberatus Mwang'ombe "Libe" ameendelea kuvunja rekodi kwa kukusanya watu wengi kuliko mgombea yeyote wa ubunge aliye wahi kutokea jimbo la Mbarali. Mh. Mwang'ombe ambaye amekuwa akiendesha mikutano yake kwa namna ya kipekee kabisa; leo, baada ya kuhutubia aliacha dakika 45 ambapo alisema "nimeomba mdahalo na mgombea wa CCM, Haroon, amekataa; nimeomba mdahalo na mgombea wa ACT, Modestus Kilufi, amekataa; sasa nawaruhusu watu wa Ubaruku mnifanyie mdahalo peke yangu."
Watu wa Ubaruku walimuuliza Mh. Mwang'ombe maswali zaidi ya 10 ambapo walipata majibu stahiki hadi wananchi wakawa wanamwambia Mh. Mwang'ombe inatosha nenda kapumzike. Moja ya maswali aliyo ulizwa Mh. Mwang'ombe ni pamoja na nini atakifanya juu ya huduma ya afya. Mwang'ombe alisema atashirikiana na madiwani, bwana afya wa wilaya na madaktari kuhakikisha wana boresha huduma za afya Mbarali. Zaidi, Mh. Mwang'ombe anaamini kuwa huduma ya afya ni haki ya binadamu; hivyo basi, serikali inawajibu wa kuhakikisha inapeleka vifaa kama, madawa, gloves, nyembe, sindano kwenye vituo vya afya.
Mh. Mwang'ombe akiendelea kutililika jukwaani
Ni nyomi
Juu na chini: umati wa watu ulio jitokeza kumsikiliza Mh Liberatus Mwang'ombe