Sunday, November 16, 2014

MWANA-DIASPORA, LIBERATUS MWANG'OMBE "LIBE", ATOA "INSPIRATIONAL SPEECH" KWA FORM FOUR

Hotuba ikiendelea
Akiongea na watahiniwa wa kidato cha nne siku mbili kabla ya mtihani wa Taifa 2014,  shule ya secondary Montfort iliyopo Rujewa, Mbarali, Mwana-diaspora na "alumni" wa Montfort Secondary kutoka Washington, D. C., Marekani,  Liberatus Mwang'ombe "Libe" alianza kwa kusema, Montfort ni shule aliyo soma na anajisikia faraja akiyaona mazingira yale.  Aliendelea kwa kusema, maamuzi ya mwisho ya kila binadamu yapo chini ya himaya yake.  Alisema "huwezi kutegemea mtu baki au mwingine aongoze au arutubishe maisha yako, ni wewe binafsi unaweza kufanya tofauti kwenye maisha yako na kila binadamu ni kiongozi.  Pia alisema anaamini kuwa kila binadamu ana ndoto zake kwenye maisha; alisema; "ni muhimu kujiwekea malengo ya ndoto zenu. Malengo ambayo yanatimilika, malengo ya kiuhalisia na malengo yenye muda maalumu." Aliendelea na kusema, "ndoto bila malengo itaendelea kuwa ndoto na kutimilizwa kwake kutaendelea kuwa ni ndoto tu."  Mwisho Ndg. Libe aliwaomba wanafunzi hao wasimuangushe kwa kuweka malengo kwenye ndoto zao na kuhakikisha wanazitimiliza.

 Mbali ya maongezi Ndg. Liberatus alichangia miundombinu ya elimu kwa wanafunzi hao
Moja ya wanafunzi akimshukuru Liberatus kwa kukumbuka alipotoka
Juu na chini Libe akiendelea kubadirishana mawazo na wanafunzi

Wednesday, November 12, 2014

CASE UPDATES: ATC Metro DMV Community vs Sandaly, Nyang'anyi, et al

Association Of The Tanzanian Community In America, Washington Metropolitan vs Sandaly, Nyang’anyi, et al

Hearing date is on Nov 26, 2014, 8:30am at Circuit Court for Howard County - Civil System. Save the date.


Financial record subpoena

We have received ATC Metro Financial Records from PNC Bank.  Two years record; since 2012 to date.  Preliminarily analysis of the record shows discrepancies.  For example, checks have been written to individuals who we doubted at the first place, debit transactions, major withdrawals prior to election, etc.  The record is concealed at this moment and shall be revealed to public when right time comes

DONATION AND MORE INFO ABOUT THIS CASE CLICK HERE
 
Thank you so much for patience and unconditional support. 

Tuesday, November 11, 2014

KATIBU WA CHADEMA DMV, USA, ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA CHADEMA TANZANIA

Katibu wa CHADEMA DMV, USA, Liberatus Mwang'ombe amefanya ziara ya kutembelea makao makuu ya CHADEMA jijini Dar Es Salaam. Kwenye ziara yake aliweza kufanya mkutano na Dr. Wilbrod Slaa na mratibu wa mambo ya wabunge CHADEMA, John Mrema. Pia Ndg. Liberatus alipata fursa ya kujadili changamoto zinazo wakabili waTanzania kwa ujumla na mbinu za kukabiliana nazo. Zaidi walijadili namna ya kutatua changamoto hizo na kuhakikisha Tanzania inakuwa ya waTanzaia na sio watu wachache.
 Juu na chini; Katibu CHADEMA, DMV, USA, Liberatus Bagasa Mwang'ombe (aliye simama) akiwa na katibu Mkuu CHADEMA, Dr. Slaa walipo kutana makao makuu
 Juu na Chini; Dr. Slaa na Liberatus Mwang'ombe wakikaa kwaajili ya picha na majadiliano