Thursday, November 5, 2015

ASANTENI SANA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI, MBARALI 2015


Kwa marafiki na wapenzi wangu wote tulio shirikiana kwenye kampeni zangu, Liberatus Mwang’ombe, za ubunge 2015 jimbo la Mbarali;



Kwanza kabisa naomba samahani kwa kuchelewa kuwashukuru wote mlio tumia muda wenu, mali zenu, na nguvu zenu kwenye kampeni hizi.  Nawashukuru kwa kunipa support ya kifedha, mawazo, vyombo, ushirikiano usio na kikomo; na kuniamini.

Natambua wazi tumepita kwenye kampeni ambazo ni ngumu na zenye changamoto nyingi, lakini hata siku moja hamkuweza kuniacha. Tulilia pamoja, tulicheka pamoja na tulifurahi pamoja na tuli huzunika pamoja.  Kuna siku zilipita bila hata kupata chakula cha mchana; lakini, kwa sababu lengo letu lilikuwa ni moja, hatukuteteleka.  Mwisho wa siku tumemaliza kampeni salama kwa uwezo wa mwenyezi Mungu.

Kwa umoja wetu tumeweza kuionyesha Mbarali, Tanzania na dunia kuwa tukiungana na kuamua kufanya kitu hakuna wa kutuzuia.  Tumefanikiwa kwa kuweza kufikia kata zote 20; na kufanikiwa kupata madiwani 8 kutoka 2 tulio kuwa nao 2010.  Kwa pamoja tulishirikiana kwa nguvu zote na maarifa yote.

Hadi tunamaliza uchaguzi matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:
Haroon Mulla (CCM) 45,352
Liberatus Mwang'ombe (CHADEMA) 36,603
Modestus Kirufi (ACT) 20,606
Gamdust Hajji (CUF) 382
Getruda Pwilla (NCCR) 120
Nurdin (UPDP) 114

Siumii kunyang'anywa ushindi Mbarali. Naumia navyo ona wakina mama, vijana na wazee wa Mbarali walio jitolea kwa moyo moja bila kulipwa kufanikisha kampeni zetu wanavyo toa machozi na kuja nyumbani wakiniuliza haki yao ipo wapi. Tunaishi kwenye nchi ambayo hata ukipiga Kura; huna hakika kama itahesabiwa, na hata kama ikihesabiwa; huna hakika kama itaenda kwa yule uliye mpigia.

Tumemaliza kampeni na uchaguzi; najua inaumiza sana, lakini ni wakati wa kurudi kwenye maisha yetu ya kawadi na kuondoa makandokando na tofauti zilizo jitokeza kipindi cha kampeni.  Sisi wote ni wamoja na naamini hakuna ambaye aliingia kwenye kampeni kwa maslai binafsi; wote tulikuwa tunapigania maslai ya Mbarali na Tanzania yetu.

Assanteni sana kwa ushirikiano, umoja na mapenzi mliyo yaonyesha kipindi cha kampeni na sasa. Nisinge fikia hapa bila ya nyinyi, kwani ili niwe mimi ni lazima nyinyi muwepo; vinginevyo “I’m nothing”.

MUNGU IBARIKI MBARALI, MUNGU IBARIKI TANZANIA


Liberatus Laurent Mwang’ombe
BAGASA2015

UJASIRI WA KUAMUA/UJASIRI WA KUTHUBUTU

No comments: