Ni Liberatus Mwang'ombe "Libe" katika ubora wake ameweza kukonga nyoyo za watu wa Mbarali na Watanzania kwa ujumla. Mwang'ombe ameingia kwa style tofauti na wagombea wengi ambao wamekuwa wakivaa kombati au sale za CHADEMA: Yeye, Mwang'ombe, alitokea halmashauri akiwa amepigilia suti nyeusi na tai nyekundu huku akiwa anakitambaa chenye rangi za CHADEMA na beji ya CHADEMA. Wana Mbarali wengi wameonyeshwa kufurahishwa na Mwang'ombe aliye onyesha style tofauti na wagombea wengi ambao wamekuwa wakivaa kombati na sare za CHADEMA. Pia, Mwang'ombe ameonekana ni mtu mwenye kujiamini na kuongea na kila mtu hapo halmashauri.
Baada ya kupokea fomu ya kugombea Ubunge Mwang'ombe alionekana akimgusa gusa bega mkurugenzi wa halmashauri huku akiongea naye na kumshukuru kwa kuwezesha zoezi hilo la uchukuaji wa fomu.
Liberatus akinyesha fomu
Liberatus akipokea fomu
Msafara
Majadaliano kabla ya makabidhiano ya form
Signing out
Kuondoka halimashauri