Monday, August 11, 2014

MCHANGANUO ZAIDI KUTHIBITISHA UCHAKACHUAJI WA UCHAGUZI WA August 9, 2014

MCHANGANUO HUU UNAENDELEA KUTHIBITISHA KUWA UCHAGUZI WA AUGUST 9, 2014 NI BATILI
"TOA KURA 15 MARUANI; LIBE ATOSHA"

Tumesoma mchanganuo wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Mzee Safari na ametoa mahesabu ambayo yanazidi kuongeza sintofahamu. Huu ni mchanganuo wa kutengenezwa ili kuwapumbaza wana DMV; “Team Libe for DMV President 2014”  itathibitish ubatilii huu pasi na shaka.  Tunanukuu mchanganuo huo wa Tume hapa chini. Kama ifuatavyo;  

Mchanganuo wa Tume ya Uchaguzi kutoka kwenye report ya mwisho.
Yafuatayo ni matokeo ya ukaguzi  wa mfumo wa kura uliobainisha hitilafu:
a)Idadi ya wapiga kura walioko kwenye orodha ya wanachama  hai:   586. Wanachama 150 waliamua kutopiga kura.
b) Wanachama waliopiga kura kituoni: 436
c) Kura za ghaibu ( in absence): 14 Mgawo wake ni:  Libe 9 na Iddi 5
d) Kura zilizo toka kwenye masanduku na kuhesabiwa na mawakala: 445:  Katika hizo mawakala wa Libe waliripoti kura 214, na wa Iddi waliripoti kura 231:  Kwa hivyo kuna kura za ziada  kwenye masanduku kuliko idadi ya wapiga kura.  Ziada hiyo ni kura 9.

           Kutokana na mchanganuo huu wa kupikwa, naomba msomaji shirikiana na “Team Libe for DMV Community 2014” ili tuthibitishe udanganyifu wa Tume ya Uchaguzi na Board of Trustee chini ya Hamza Mwamoyo.
            Mzee Safari anasema; Wanachama hai ni 586, wanachama ambao hawakupiga kura ni 150; na waliopiga kura kituoni ni 436.  Mzee Safari anaongeza kuwa; waliopiga kura za ghaibu (absentee ballot) ni 14.
            Sasa basi, shirikiana nasi kufanya mahesabu ya darasa la kwanza kwa kujumlisha waliopiga kura kituon 436, ambao hawakupiga kura 150 na waliopiga kura za ghaibu (absent) 14; (436+150+14= 600).  Rejea hapo juu orodha ya wanachama hai ni 586, lakni jumla inaonyesha 600: KWA NINI NUMBER STILL DON'T ADD UP!

Ukichukua kura za ziada 9 (445-436=9) ongeza na wanachama ambao sio hai 14 unapata kura maruhani 23  (9+14).   Hii inamaanisha uchaguzi huu ulikuwa na kura BATALI 23. 

Napenda kuitaarifu Board of Trustee na Tume ya Uchaguzi kuwa; wana DMV 223 walio mchagua Liberatus (50% ya walio piga kura) bado wanaomba maelezo juu ya kura 15 batili; na sasa tunaomba maelezo ya kura 23 BATILI.  Pia, kulingana na mchanganuo huo hapo juu; inaonyesha kuna watu 14 ambao sio wanachama hai walishiriki kupiga kura.   UCHAGUZI HUU NI BATILI KAMA ALIVYO SEMA MZEE SAFARI SIKU YA JUMAMOSI AUGUST 9, 2014; TUNAOMBA WANA DMV MSHIRIKIANE NASI KATIKA KUDAI HAKI KWA KUWEKA SAHIHI KWENYE PETITION HII PINGA UCHAGUZI WA AUGUST 9, 2014 NI BATILI


TEAM LIBE FOR DMV COMMUNITY PRESIDENT 2014


UCHAGUZI DMV: WEKA SAHIHI KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI WA AUG 9, 2014

WE NEED TO SHARE AND SIGN THIS PETITION. WE CAN'T JUST TALK THE TALK, CLICK HAPA KUPINGA UCHAGUZI WA AUGUST 9, 2014 

Maswali muhimu
 -Kwa nini Ndg. Hamza kaja na matokeo after 24hrs ambayo katuongezea kura moja moja wagombea bila kushirikisha wakala

- Kura 15 zilitoka wapi (hizi kura have change the whole election kwani Idd anaongoza kwa kura 13)

-Kwa nini Hamza Mwamoyo atoe matokeo badala ya Tume ya Uchaguzi.  Ngd. Hamza ana mamlaka gani yakutoa matokeo na yeye sio mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi?

-Mwenyekiti wa Tume alikataa kutangaza matokeo na kusema uchaguzi ni VOID siku ya uchaguzi. Alilazimishwa kutaja mshindi. ALIKATAA.

-Kwa nini Hamza akatae "re-count" na kuondoka na kura kwenda nazo kusiko julikana?

-Hadi jana Aug 10, 2014 Mzee wetu Safari ambaye ni M'kiti wa Tume ya Uchaguzi hakutangaza mshindi 

-Hamza Mwamoyo ana mamlaka gani ya kutangaza matokeo na yeye sio M'kiti wa Tume ya Uchaguzi

-Mwisho, kuna conflict of interest; Hamza Mwamoyo ni mwenyekiti wa Board ya TAMCO na Idd Sandaly alikuwa M'kiti na Treasury wa TAMCO

Team Libe 223 (50% of the voters) supporters voice MUST BE HEARD

WE NEED TO SHARE AND SIGN THIS PETITION. WE CAN'T JUST TALK THE TALK, CLICK HAPA KUPINGA UCHAGUZI WA AUGUST 9, 2014 

Maswali, uliza hapa

Mwanaid Love "Mona" / Campaign Manager   202-374-2666

Omby nyongore /Camapaign Ass.  Manager     240-595-5100

Alawi Omari / Campaign Strategist                  301-339-3765

Amri Maliyatabu / Adviser                                240-426-8271

Liberatus Mwangombe/Libe                              240-423-3331

Imetolewa na Team Libe for DMV Community 2014

Sunday, August 10, 2014

TEAM LIBE FOR DMV COMMUNITY: UCHAGUZI WA August 10, 2014 NI BATILI

Ni masaa 24 yamepita toka uchaguzi ufanyike huku Tume ya Uchaguzi bado imekuwa na kigugumizi kutoa msimamo na kutangaza matokeo.  Uchaguzi huu uliofanyika August 9, 2014 umedhihirika pasi na shaka kuwa ni BATILI.  Baadhi ya mambo yanayofanya uchaguzi huu ni batili na “Team Libe for DMV President 2014” inaweka wazi msimamo wake kuwa, HATUTAKUBALI MATOKEO YEYOTE YATAKAYO TOLEWA NA TUME KWA SASA KWANI UCHAGUZI HUU NI BATILI “FRAUD ELECTION”.

Baadhi ya sababu zinazo batilisha uchaguzi huu ni kama zifuatazo;
Moja,  jumla ya watu walio piga kura ilikuwa 430 huku Idd Sandaly alipata jumla ya kura 231 na Liberatus kura 214.  Ukijumlisha kura za Liberatus na Idd unapata kura 445, yaani kura maruhani ni 15 (214+231=445).  Hii ina maanisha kuwa, Liberatus alipata 49.76% na Idd alipata 53.72% ya kura zilizo pigwa. Ukijumrisha hizi asilimia unapata 103.48% (53.72+49.79= 103.48%).  Hii ni bila kuweka “absentee ballot. Ukiweka absentee ballot Liberatus ana kura 222 ambayo ni 51.62% ya kura zilizo pigwa na Idd ana 235 ambayo ni 54.65% ya kura zilizo pigwa.  Hii ina maanisha ukijumrisha jumla ya asilimia za Idd na Liberatus unapata 106.27% (51.62%+54.65%).  Hii haileti maana yeyote kama wagombea wote wana kura zaidi ya asilimi 50% ya zilizopigwa; UCHAGUZI HUU NI BATILI.

Pili, baada ya mkanganyiko huu kutokea, wakala wa Liberatus hakuyakubali matokeo na wala hakuweka sahihi.  Aliomba kura zihesabiwe tena; alikataliwa.  Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi baada ya kuona mkanganyiko huu alitamka kuwa uchaguzi huu ni “VOID” na hawezi kumtangaza mshindi.  Mzee Safari alishinikizwa na baadhi ya watu wa Board of Trustee akiwepo Ulotu, baadhi ya watu wa Tume ya Uchaguzi na mashabiki wa Idd Sandaly atangaze matokeo. Mzee Safari alisema hatotangaza matokeo na kama mnataka kutangaza; chukueni mic hii hapa.  Baada ya mtafaruku huu, Mwenyekiti wa Board of Trustee, Hamza Mwamoyo, alimuita Mzee Safari faragha. Baada ya Mzee Safari kurudi alisema “sitatangaza mshindi bali nitatangaza numbers”. Hadi leo hii Jumapil, August 10, 2014, 9pm hakuna mshindi aliyetangazwa wala Tume haijatoa neno. UCHAGUZI HUU NI BATILI.

Tatu, mwenyekiti wa Board of Trustee, Hamza Mwamoyo, alizichukua kura zote akimuahidi wakala wa Liberatus kuwa tutafanya “re-count” na akamuagiza amwambie Liberatus anipigie simu ili tuone tutafanya vipi “re-count”.  Liberatus alimpigia simu Hamza Mwamoyo zaidi ya mara tano bila majibu.  Mzee Mwamoyo alitokomea na kura zile kusiko julikana.  Hadi walaka huu unaandikwa baada ya masaa 24; Ndg Hamza Mwamoyo hajarejesha simu ya Liberatus.  Swali la kimsingi ni kuwa; inakuaje kura za makatibu zilifanyiwa “re-count” na gap yake ilikuwa kubwa kuliko kura za marais na za marais zikataliwe kufanyiwa re-count? UCHAGUZI HUU NI BATILI

Nne,  watu waliopiga kura walikuwa 430, kura za makamu wa Rais zilikuwa kama ifuatavyo; Heriet Shangarai kura 333 na mama Salma Moshi kura 94. Ukijumrisha hizi kura unapata jumla ya 427 (333+94).  Matokeo haya bado yapo chini ya jumla ya watu waliopiga kura 430 (let say kura 3 ziliharibika).  Wakati kura za maraisi jumla yake ilikuwa 445; je kura 15 zilitokea wapi? Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi, Asha Nyang’anyi, amekili kuwa kuna kura ziliharibika na wala hakusema ni ngapi. Alisema nyingi.  Baada ya kumbana sana aliendelea kusema nyingi bila kuwa “specific” ni kura ngapi ziliharibika.  Hata kama kuna kura nyingi zilizo haribika; bado zitakuwa zinaenda nje ya kura halali 430.  

Kura za katibu zilikuwa kama ifuatavyo; Said Mwamende alipata kura 251 na Ismail Mwilima alipata kura 171.  Ukijumrisha kura hizi unapata jumla ya 422 (251+171). Bado kura za makatibu zipo chini ya jumla ya wapiga kura walio tokea 430; hii inamaana kura 8 ziliharibika.  Je, ni kwa nini za marais zilizidi kura 430 hadi kufikia kura 445? Kura 15 zilitokea wapi?.  Makamu wa katibu Bernadeta Kaiza alipata kura 254 na Solomn Cris alipata kura 167; jumla ya kura hizi ni 421 (254+167).  Bado na hizi zipo chini ya jumla ya watu walio kuja 430; hii inamaana kura 9 ziliharibika. Kwa nini za maraisi zinazidi watu walio kuja?  UCHAGUZI HUU NI BATILI

Tano, Ndg. Idd Sandaly amekuwa akijitangaza kuwa yeye ni mshindi na leo hii jumapili August 10, 2014 alikuwa kwenye mkutano wa CCM akijitangaza kuwa yeye ni Rais wa DMV.  Je, Idd amejuaje kuwa yeye ni Rais mpya wa DMV ilihali Tume bado haijatangaza mshindi?

Kwa hoja hizi tajwa “Team Libe for DMV Community President 2014” inapenda kuchukua fursa hii kuutangazia Umma wa DMV na wapenzi wake 222 yaani 51.62% ya wapiga kura kuwa:  HATUTA TAMBUA MATOKEO YEYOTE YATAKAYO TANGAZWA NA TUME JUU YA UCHAGUZI HUU BATILI.  “Team Libe for DMV Community President 2014” bado inaamini Board na Tume ya Uchaguzi watatumia busara kutatua mgogoro huu ili tuwe na jumuia isiyo na mpasuko.  Pia, wahusika watambue kuwa; Team Libe ina watu zaidi ya 222 (51.6% ya walio piga kura 430) ambao wanahitaji kupewa majibu stahiki.  Ustawi wa jumuia upo mikonpni mwa Tume ya Uchaguzi.   Nawahasa watu wa Team Libe for DMV president wawe na uvumilivu huku tukisubiri kauli ya Tume ya Uchaguzi.

Imetolewa August 10, 2014
Mwanaid Love “Mona”/ Campaign Manager

UNITED WE STAND; DIVIDED WE FALL

TAMKO: TEAM LIBE FOR DMV COMMUNITY PRESIDENT 2014 JUU YA UCHAGUZI

Baada ya muda wa ukumbi kuisha na kura zikiendelea kuhesabiwa: matokeo yalikuwa kama ifuatavyo;

Urais
Idd Sandaly kura 231
Liberatus Mwangombe Kura 214
Jumla ya watu walio piga kura ilikuwa 430
Hii inamaanisha Idd amepata 53.7% ya kura zilizo pigwa na Liberatus amepata 49.76% ya kura zilizo pigwa. Ukijumrisha hizi asilimia, unapata 107.89%. Swali; 7.89% imetoka wapi?

Ukijumlisha kura za Idd na Liberatus 231 +214= 445.  Hii inaonyesha tofauti ya kura 15 huku Idd akiongoza kwa kura 17. Hii inamaanisha kulikuwa na kura za ziada 15, yani kura 15 zilikuwa hazijulikani zilipo toka. 

Wakala wa Liberatus alipewa kura 8 za absentee ballots na wakala wa Idd alipewa kura 4 za absentee ballots.  Tatizo hapa; hatukupewa idada ya watu walio piga absentee ballot na wala hawakusema ni ngapi zimeharibika.

Ukijumrisha kura za ukumbini na absent ballot, matokeao ni;
Idd Sandally 231+4= 235
Liberatus Mwangombe 214+8= 222
Hii inaonyesha Idd anaongoza kwa kura 14

Swali kuu ni kuwa; Zile kura 15 zilizo zidi zime tokea wapi?

Baada ya kuona mapungufu haya kwenye kura; Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Ndg. Safari alitamka kuwa uchaguzi huu ni “VOID” na hawezi kutangaza mshindi; lakini atatangaza numbers. ALITANGAZA NUMBERS ZA UWANJANI TU, HAKUTANGAZA ABSENT BALLOT.  Wakati sintofahamu hili likienedelea; “Team Libe for DMV Community President” iliomba “re-count”; ikashindikana kufanya re-count baada ya polis kuchukua mic na kufukuza kila mtu ukumbini.  Watu wote walitoka ukumbini ndani ya dakika moja.  Ikumbukwe; ukumbi ulichukuliwa hadi saa nne usiku.  Wakati tunafukuzwa na polis ilikuwa ni saa tano usiku.  Mwenyekiti wa Board Ndg. Hamza Mwamoyo aliondoka na kura zote akidai tutafanya re-count.

Kipengele kingine ambacho kilikuwa na utata ni cha makamu wa Rais. Ieleweke kuwa; box la makamo wa rais na Rais lilikuwa moja. 

Nafasi ya makamu wa Rais matokeo yalikuwa kama ifuatavyo;
Heriet Shangarai kura 333
Salma Moshi kura 94
Ukijumrisha matokeo ya makamu wa raisi unapata jumla ya kura 429.  Hii bado inaonyesha ukakasi; kwa nini kura za Rais ziwe jumla 445 na makamu 429 na zote zimetoka kwenye box moja; na karatasi linalo tumika kupigia kura lina katwa sehemu mbili, ya juu ni ya Rais na chini ya Makamu wa rais; zote zinaingia kwenye box moja.  Hoja; kwa nini number za makamu wa Rais na Rais don’t add up! Au, kwa nini number za mgombea wa makamu wa mwenyekiti  zime “match” na wapiga kura; wakati number za raisi hazijamach na zote zinatokea wenye box moja (zinatofauti ya kura 16)?

Itambulike kuwa; msimamo wa “Team Libe for DMV Community President 2014” unaamini Board na Tume ya Uchaguzi watatumia busara kutatua mgogoro huu ili tuwe na jumuia isiyo na mpasuko.  Pia, wahusika watambue kuwa; Liberatus ana watu zaidi ya 222 (51.6% ya walio piga kura 430) ambayo ni  walio mpigia kura ambao wanahitaji kupewa majibu stahiki.  Ustawi wa jumuia upo mikonpni mwa Tume ya Uchaguzi.   Nawahasa watu wa Team Libe for DMV president wawe na uvumilivu huku tukisubiri kauli ya Tume ya Uchaguzi.

Imetolewa August 9, 2014
Mwanaid Love “Mona”/ Campaign Manager

UNITED WE STAND; DIVIDED WE FALL

Saturday, August 9, 2014

BREAKING NEWS: MORE CREDIBLE AND PROFESSIONAL ENDORSEMENTS: 2nd MEDICAL DOCTOR ENDORSES LIBERATUS MWANGOMBE FOR


Naitwa Dr Allan,MD., MPH. Naipenda Jumuia yetu ya DMV na napenda sana kuona mabadiliko chanya katika mambo mbali mbali yanayotuhusu na yanayoihusu Jumuia yetu. Kwa sasa nipo Tanzania, Kura yangu through absentee ballot (procedures zote zimeshafuatwa) imeenda kwa Liberatus MwangOmbe(urais) na Solomon(Katibu msaidizi), Hawa sii tu kwamba ni watu ninaowafahamu na tuliobahatika kwenda same high school (Tambaza) japo kwa vipindi tofauti-BALI wameweza kujipambanua kwa ufasaha na kwa kutumia simple and clear non abusive language kujenga hoja makini na zenye MASHIKO katika kutengeneza sera na miongozo tarajiwa-katika kuipeleka jumuia yetu to the "next level". 

Kikubwa ambacho hatuhitaji chaki au daftari na kalamu kueleweshwa ni INCLUSIVE INVOLVEMENT/PARTICIPATION OF EVERY COMMUNITY MEMBER katika kila jambo linalotuhusu kama Jumuia, hii nia dhahiri ya UWAZI ni alama tosha ya nia njema kwa jamii na Jumuia yetu, kitu ambacho Jumuia yetu kwa miaka mingi tulikikosa na kusababisha kupoteza imani kwa Viongozi wa Jumuia, na Jumuia kwa ujumla-kwa watanzania wengi wa DMV.

Shime wana DMV, SOLUTION YA KUUJENGA UPYA NA KUUIMARISHA UPYA UMOJA WETU NI "LIBE+His Cabinet" PEKEE! Hivyo basi, Wakati wa mageuzi ni sasa, naomba tuwape support na tujitokeze kuwapigia kura watu hawa ili tusonge mbele kwa ustawi BORA wa sasa na wa baadae wa Jumuia yetu.

VOTE FOR LIBE AND SOLOMON FOR POSITIVE INNOVATIVE CHANGE!!

Friday, August 8, 2014

OFFICIAL STATEMENT: TEAM LIBE FOR DMV COMMUNITY PRESIDENT 2014 INASISITIZIA MDAHALO

UCHAGUZI DMV NA MDAHALO TEAM LIBE FOR DMV COMMUNITY 2014
Baada ya mahojiano na Jamii Production ikishilikiana na Vijimambo Blog yaliyo fanyika Ubalozini Wshington D.C. August 8, 2013 na Liberatus Mwangombe; kumekuwa na malalmiko kuwa Ndg. Idd Sandaly hakuwa na fursa ya kujibu shutuma.  “Team Libe for DMV Vommunity President 2014” bado inasisitiza kuwa ipo wazi kwa debate (mdaharo)

Tuna masaa zaidi ya 15 hadi uchaguzi utakao fanyika kesho mchana kuanzia saa 8 (2pm); hivyo basi, “Timu Libe for DMV Community President 2014” tupo wazi kwa mdaharo hata Jumamosi asubuhi kabla ya uchaguzi.  Tunaomba kwa ukarimu na moyo wa dhati Ndg. Bandio na DJ Lu (Lucas) kama wanaweza kuwezesha mdaharo huo leo jumamosi asubuhi watujurishe; tutashiriki bila kikwazo.

UNITED WE STAND; DIVIDED WE FALL
 Omby Nyongore/ Assistance Campaign Manager

JUST IN: UCHAGUZI DMV: DOTTO HAROUN ENDORSES LIBERATUS MWANGOMBE FOR DMV PRESIDENT

Mimi Dotto Haruna nimeamua kusimama na Liberatus Mwangombe kwenye huu uchaguzi kwa sababu Libe ni MUWAZI, MKWELI, HAMUNG'UNYI maneno kwenye ukweli wala hana upendeleo. Naomba wana DMV mniunge mkono kwenye kumpa Libe fursa

KAMA ANAVYOSEMA BI MOZA "LIBE ATOSHA"

KAMA ANAVYOSEMA BI MOZA "LIBE ATOSHA"

BREAKING NEWS: MORE ENDORSEMENT FOR LIBE: JASON MATOLELA ENDORSES LIBERATUS MWANGOMBE

I, Jason Mtolela endorsing Liberatus Mwang'ombe for the Association of Tanzanian Community (ATC) DMV president 2014

    By the way, I should be clear that I am an independent; I don't have any political affiliation with any ideology. For more than a decade I have lived in DMV area, but I never voted for any ATC president, this will be my first time to walk to the ballot box to cast my vote. Our past community leaderships have been characterized with serious corruption, failure to unity the community, using community leadership to advance personal interests, failure to address the core needs of the community, among the others. According to my survey, such attitudes or behaviors of our leaders have been recipe for community disunity and dysfunctional.


       Recently, I have been closely following our community campaign trail. I made up my mind that decision not to cast my vote is not a good option at this time, as by doing so is giving up on my own life and a bright future. As we all know as a community, we all have an extraordinary stake at this election. So, I decided that this time around I have to participate in our legitimate election for the leadership of our community, which is an essential component for our progress, not only over here in the DMV, but also back in our homeland.

        As aforementioned, I am an independent, and I don't have any intention whatsoever to demean Idd Sandaly with his outgoing team. This leadership has failed to achieve the main objectives of our community in many aspects. I will catalog a handful of those failures: it failed to unity members of our community, if the statistics indicating that there  were less than ten active members until the time of election is true, then the community is in a serious situation, because, if such disunity continues unchecked will lead to the collapse of ATC. 

       Unaccountability on community funds is another failure. It doesn't make sense when the outgoing leadership claims that it cannot disclose the ATC financial records. it should be remembered that the leadership has been put in the office by the members, who voted for it, and that they (members) have the right to have access to such records. The question to every community member is: will I vote for someone who is hiding financial records from the members?

       Idd Sandaly with his team failed to demonstrate transparency.  Community members deserve more than what this leadership has done. Many issues during this leadership were dealt with behind closed doors. No adequate information were given to members. Such behavior led to mistrust of the leadership. This atmosphere is not favorable for the prosperity people are looking for.

        We need transformation in our community. The leadership is intended to be a vehicle through which our dreams can be fulfilled. So, as voters, we need someone who will be a trustful leader, uniting figure, transparent, visionary and one who will address our needs not wants. This is Liberatus Mwang'ombe.

        As we all know, the society is dynamic, so we need a leader who will bring us together for our collective objectives so we can chart a new course, and  Libe has demonstrated that. He has ignited the desire and passion people has been waiting for, for a long time. So many of our fellow community members have great ideas, but have been shut outside by our leaders. His policies are consistent with our needs; what we need is to use our fundamental rights (vote) to propel him to the office.

       Liberatus's policies indicate that he will not only be responsible for our community here in DMV, but to connect us to our homeland as well. He is a staunch advocate for our National Constitutional amendments, that will facilitate our development and our fellow Tanzanians.  Libe has unique leadership potentials; as a community we need to utilize him for our development economically, socially and in other aspects.

I am asking for our community brothers and sisters to vote for Libe, a transformational and uniting figure.


Jason Mtolela