Juu na chini akiwa Ubaruku. Chini anachukua maswali baada ya mkutano
Ni Liberatus Mwang’ombe “ Libe”, au
kama watu wa Mbarali wanavyo muita “Mnyamwezi” aliye wahi kukaaa DMV (DC,
Maryland na Virginia) ameendelea kuwa gumzo kwenye mbio za Ubunge jimboni
Mbarali. Mwang’ombe amekuwa akivunja
rekodi kwa kila mkutano anao fanya; amekuwa anakusanya watu wengi sana kuliko kipindi
chochote cha ubunge jimboni Mbarali
Uwezo wa Mwang’ombe kutoa hotuba za
umoja, ushirikiano na bila kuweka uchama imekuwa chachu na kigezo cha kuwavuta
wana Mbarali wengi. Zaidi, Mwang’ombe amekuwa akiongea na watu wa
kila aina hadi wa CCM ambao ndio mahasimu wake kisiasa: amekuwa akiwafuata CCM
na kuwapa mikono kitendo ambacho kimekuwa kikiwashangaza watu wengi. Kumekuwa na kasumba ya watu wa CCM na CHADEMA
kuto kusalimiana na kuogopana kipindi cha kampeni; tofauti na Mh. Mwang’ombe
ambaye amekuwa akipita hadi kuwasalimia watu wa CCM hata kama yeye ni CHADEMA.
Watu wa kila pande ya jimbo la
Mbarali wamekuwa wakizungumza kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano ya Mh.
Mwang’ombe; huku wengine wakisukuma gari lake baada ya mikutano, wengine wakimzuia
barabarani hadi ashuke ili wamuone, wengine wakitaka atembee nao barabarani
kuonyesha umoja na mshikamano.
Liberatus Mwang’ombe anaomba msaada
kwa waTanzania wote, diaspora na waliopo nchini, wamsaidie kufanikisha harakati
za kwenda DODOMA.
Mh. Mwang’ombe anaomba michango ya kifedha ambayo inaweza
tumwa kupitia WAVE-App, M-Pesa number +255 752 494
409
Au kama una mchango na huna
WAVE-App wasiliana na
Rehema 301 367 9711
Jabil 240
604 0574
Lukresia 240 593 5973
Kwa picha zaidi endelea kurasa ya pili